• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 5:36 PM
Kesi ya Mwilu yaibua kero la uchaguzi 2017

Kesi ya Mwilu yaibua kero la uchaguzi 2017

Na PETER MBURU

KUFIKA kortini kwa naibu wa Jaji Mkuu Philomena Mwilu na mawakili tajika zaidi  kumtetea baada yake kukamatwa jana kumeibua tena kumbukumbu za kesi ya kihistoria iliyopelekea kufutiliwa mbali kwa ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta 2017.

Alipowasili kwenye mahakama za milimani Jumatano asubuhi, Bi Mwilu aliwakilishwa na mawakili wenye sifa za kushinda kesi wakiongozwa na James Orengo aliyeongoza kikosi cha mawakili waliobwaga uchaguzi wa Rais Uhuru Kenyatta.

Mawakili wengine kama Harun Ndubi, Okong’o Omogeni, Kalonzo Musyoka, John Khaminwa, Peter Kaluma, Edward Waswa, Mutula Kilonzo Jr na Nelson Harvey aidha wako kwenye orodha ya watetezi wa naibu wa jaji mkuu akiwa kizimbani.

Kilipoanza kikao cha kusikizwa kwa kesi hiyo, mawakili wa Bi Mwilu wakiongozwa na Bw Orengo walianza kwa kutoa hoja kuwa kesi iliyo mbele ya korti si ya jinai, hivyo wakiitaka mahakama kuamua hivyo.

“Ni jukumu la korti kuamua kuwa kesi hii ni ya civil wala si ya jinai, wala haiwezi kuwachia jukumu hilo mawakili wa mshtakiwa wala idara za DPP na DCI,” Bw Orengo akaeleza korti Jumatano.

Bw Orengo alizidi kueleza korti kuwa mashtaka aliyofikishwa nayo mbele ya korti Bi Mwilu ni njia ya mumwondoa ofisini, hivyo akipinga mashtaka hayo.

Hata hivyo, huku kikao cha kesi hiyo kikiendelea kortini JajiDavid Maraga alikataa kuzungumzia suala hiloa DPP Noordin Haji alikuwa amemfahamisha kuhusu kukamatwa kwa Bi Mwilu.

You can share this post!

SOKA SAFI AU MATOKEO? Kiini cha Mourinho kukaangwa na...

Simbas yaanza kujipanga kwa mchujo kufuzu kwa Kombe la Dunia

adminleo