• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Malema mbioni kuidhinisha Kiswahili kiwe lugha rasmi ya Afrika

Malema mbioni kuidhinisha Kiswahili kiwe lugha rasmi ya Afrika

MASHIRIKA NA PETER MBURU

KIONGOZI wa Chama cha Kupigania Haki za Kiuchumi (EFF) nchini Afrika Kusini, Bw Julius Malema (pichani) sasa anataka kuidhinishwa kwa matumizi ya lugha moja barani Afrika, akidokeza kuwa Kiswahili ndiyo lugha itakayofaa zaidi.

Malema alisema hayo wakati wa kikao na wanahabari, kilichoandaliwa na chama cha EFF ambapo alizungumzia masuala mengi, likiwemo lile la Rais wa Marekani Donald Trump kuchapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kuhusu masuala ya ardhi ya Afrika Kusini.

“Sharti tuwe na lugha moja ambayo inaweza kutumiwa katika bara zima kama Kiswahili ikiwa kinaweza kukuzwa kuwa lugha ya bara,” Bw Malema, mlumbi tajika nchini humo na barani akasema.

Alieleza kuwa kuna umuhimu kuanza kuchukua hatua hizo ambazo zitafaa katika kuunganisha bara hili.

Lugha ya Kiswahili ndiyo ya pekee ya humu baraniambay inazungumzwa na mataifa mengi, hasa yale ya Afrika Mashariki na Kati, ikiwa lugha rasmi mataifa ya Kenya na Tanzania.

Takriban watu milioni mia moja wanaweza kuzungumza kwa Kiswahili, hii ikiiweka juu katika orodha ya lugha zinazozungumzwa na watu wengi, kuliko Kikorea na Kiitaliano.

Kiswahili aidha ni lugha rasmu katika muungano wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika kikao hicho, Malema aidha aliitisha kuunganishwa wa Afrika, akipendekeza kuwepo pesa za aina moja ambazo zitatumika barani kote, Rais wa bara na bunge la bara.

You can share this post!

Wafungwa 400 watoroka jela

TEKNOLOJIA: Watoto wa Mombasa wanavyounda programu za...

adminleo