• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 5:46 PM
Shule ya Padre yafungwa kwa dhuluma za kimapenzi na mihadarati

Shule ya Padre yafungwa kwa dhuluma za kimapenzi na mihadarati

Na Geoffrey Anene

Shule ya Upili ya mseto ya Caritas Mariana kutoka kaunti ndogo ya Thika, kaunti ya Kiambu imefungwa na Wizara ya Elimu kutokana na dhuluma za kimapenzi na itikadi kali za kidini.

Hata hivyo, ripoti zaidi zinasema wazazi wa wanafunzi katika shule hiyo wanadai kwamba wizara hiyo ina njama ya kunyakua ardhi ambayo shule shule hiyo imejengwa.

Mmiliki wa shule hiyo ni Padre Mkatoliki Bertrand Maria Nwochukwu kutoka Nigeria, ambaye pia anatuhumiwa kwa biashara ya mihadarati na kuajiri walimu ambao hawajaidhinishwa kufanya kazi ya ualimu.

Mkurugenzi wa Elimu katika kaunti ndogo ya Thika, Ronald Mbogo, amenukuliwa Jumatano akisema kwamba madai dhidi ya shule hiyo ni “mabaya sana.”

Inasemekana shule hii imekuwa ikichunguzwa kwa muda baada ya ripoti inajihusisha na biashara za kutatanisha. Kw amujibu wa tovuti ya Punch, uchunguzi wa afisi ya elimu katika kaunti ndogo ya Thika ulithibitisha madai hayo na sasa afisi hiyo imeanzisha mipango ya kuhamishia wanafunzi 72 katika shule zilizo karibu.

Si mara ya kwanza shule hii iliyoanzishwa mwaka 2004 imemulikwa. Mwaka 2016, ilifungwa baada ya mwanafunzi mmoja kutoka shule ya msingi ya Caritas Mariana kufariki pamoja na ripoti za unyanyasaji wa watoto na dhuluma za kimapenzi kuibuka.

You can share this post!

Mwanafunzi aitishwa mbuzi kwa kula nyama ya wenzake

Mchina aliyetusi Uhuru na kuita Wakenya ‘nyani’...

adminleo