• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:03 PM
Zimbabwe yapiga marufuku mikutano ya umma Chamisa akipanga kujiapisha

Zimbabwe yapiga marufuku mikutano ya umma Chamisa akipanga kujiapisha

BBC Na PETER MBURU

Polisi nchini Zimbabwe wamepiga marufuku mikutano ya umma katika Jiji kuu la Harare kufuatia hofu dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu, ambao tayari umeua watu 21 na zaidi ya 2,000 kuambukizwa.

Hii imekuja siku moja baada ya serikali ya nchi hiyo kutangaza hali ya hatari kufuatia kusambaa kwa ugonjwa huo ambao unakisiwa kuenea kutokana na maji ya mabwawa mawili.

Vilevile, habari hiyo imetolewa wakati kiongozi wa upinzani nchi hiyo anapanga kuandaa hafla ya umma Jumamosi kujiapisha kuwa Rais.

Baraza la uongozi wa Jiji la Harare limekuwa na matatizo ya kuwasambazia wakazi maji katika baadhi ya maeneo kwa zaidi ya mwongo, jambo ambalo limewalazimu watu kutafuta maji ya kisima na mabwawa.

Lakini raia nchi hiyo wamebaki kushangaa ikiwa marufuku hiyo itazuia makongamano mengi ya umma ambayo hufanyika kama ibada za dini na mikutano ya kisiasa.

Kwenye mtandao wa Twitter ripota wa BBC, Stanley Kwenda @stanleykwenda alisema “Serikali Zimbabwe @PoliceZimbabwe imepiga marufuku vikao vyote vya umma katika Jiji Kuu #Harare kwa sababu ya kusambaa kwa #CholeraOutbreak. Je, hii inahusisha hata kanisa, michezo ya kandanda, maonyesho ya muziki, mikutano ya kisiasa na harusi?”

Taifa hilo liliwahi kukumbwa na pigo la maambukizi ya ugonjwa huo mnamo 2008 wakati zaidi ya watu 4,000 walikufa, wakati uchumi ulidorora na sekta ya afya kulemaa.

Mkuu wa upinzani Zimbabwe Bw Nelson Chamisa alikuwa amepanga kuandaa mkutano wa umma Jumamosi ili kujiapisha kuwa Rais, akisusia ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa baada ya uchaguzi wa Julai.

You can share this post!

Majonzi Koffi Annan akizikwa

Apple yazindua simu ghali zaidi, iPhone XS Max

adminleo