• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 10:21 AM
Kisa cha maiti za watoto kupatikana kwa maboksi Pumwani chachunguzwa

Kisa cha maiti za watoto kupatikana kwa maboksi Pumwani chachunguzwa

Na PETER MBURU

SHINIKIZO zimedidi kutolewa kutoka pande tofauti kwa uchunguzi kufanywa kuhusu kisa ambapo Gavana wa Nairobi Mike Sonko alifumania maiti 12 za watoto wa kuzaliwa zikiwa zimefishwa katika karatasi.

Jumatatu, Kiongozi wa Mashtaka ya Umma (DPP) aliamrisha idara ya ujasusi (DCI) kuanzisha uchunguzi wa mara moja ili kubaini mazingira ambapo watoto hao walikufa, na sababu ya kufichwa.

DPP Noordin Haji alielekeza DCI kufanya uchunguzi na kumpokeza ripoti ya visa hivyo ndani ya siku saba.

Wachunguzi wa DCI walifanya kikao cha dharura kuhusiana na suala hilo, huku waziri wa afya Sicily Kariuki naye akishinikiza baraza la madaktari na wahudumu wa afya kuchunguza kisa hicho na kutoa ripoti ndani ya saa 24.

“Nimeelekeza @Kmpdb Interact @NCKenya na baraza la madaktari wa kliniki kufanya uchunguzi wa haraka katika kisa cha vifo vya watoto 12 wa kuzaliwa katika hospitali ya Pumwani na kutoa ripoti ndani ya saa 24 @MOH Kenya,” akasema waziri Sicily, kupitia mtandao wake wa twitter Jumatatu.

Shinikizo hizi zilikuja saa chache baada ya Gavana Sonko kufumania maiti hizo zilizokuwa zikifichwa badala ya kupelekwa mochari, katika kisa kilichogubikwa na giza totoro.

Gavana huyo alituma nyumbani bodi ya hospitali hiyo pamoja na daktari wake mkuu Dkt Catherine Mutinda na mkurugenzi Zaddock Angahya na kumteua Dkt Simon Mueke kuwa kuwa daktari mkuu mpya.

Aidha, Wakenya walizidi kutoa shinikizo zaidi haswa kupitia mitandao ya kijamii na kueleza ghadhabu zao kuhusiana na kisa hicho, huku kina mama waliojifungua katika kifaa hicho cha afya wakielezea matatizo waliyopitia.

“Nimetatizwa sana na kisa ambapo kakangu na mkewe walipata pacha katika hospitali ya Pumwani, kisha baadaye wakaelezwa kuwa watoto wote waliaga dunia. Watoto hao walizaliwa vyema wote wakiwa na uzani wa kilo 3.1 lakini hadi sasa hawajajua sababu ya kifo chao,”akasema mmoja wa Wakenya wengi.

You can share this post!

Kiswahili sasa kufundishwa nchini Afrika Kusini

ICC yamtupa Bemba jela mwaka mmoja

adminleo