• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Orodha ya wanaowania tuzo za FIFA

Orodha ya wanaowania tuzo za FIFA

Na GEOFFREY ANENE

MWANASOKA bora duniani wa mwaka 2018 atajulikana kutoka orodha ya Cristiano Ronaldo, Luka Modric na Mohammed Salah wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) litakapotangaza mshindi wa tuzo hii ya kifahari jijini London nchini Uingereza mnamo Septemba 24, 2018.

Ronaldo anapigiwa upatu kutwaa taji hili. Mshambuliaji huyu kutoka Ureno amewahi kushinda tuzo hii mwaka 2008, 2013, 2014, 2016, 2017. Alimaliza katika nafasi ya pili mwaka 2009, 2011, 2012 na 2015 nyuma ya mvamizi matata wa Argentina Lionel Messi. Nafasi mbaya Ronaldo amewahi kumaliza katika tuzo hizi baada ya kuorodheshwa kama mwaniaji ni nambari tatu mwaka 2007 nyuma ya mshindi Kaka (Brazil) na Messi.

Kuna vitengo tisa katika tuzo hizi za kila mwaka za FIFA ambapo washindi watajulikana leo Jumatatu.

 

VITENGO NA WAWANIAJI

Mwanasoka bora wa mwaka duniani (mwanamume): Cristiano Ronaldo (Juventus/Real Madrid), Luka Modric (Real Madrid) ama Mohamed Salah (Liverpool)

Mwanasoka bora wa mwaka duniani (mwanamke): Ada Hegerberg (Lyon), Dzsenifer Maroszan (Lyon) ama Marta (Orlando Pride)

Kocha bora wa mwaka duniani: Didier Deschamps (Ufaransa), Zinedine Zidane (Real Madrid) ama Zlatko Dalic (Croatia)

Kipa bora wa mwaka duniani: Thibaut Courtois (Real Madrid/ Chelsea), Hugo Lloris (Tottenham) ama Kasper Schmeichel (Leicester City)

Bao safi (Fifa Puskas Award): Gareth Bale (Real Madrid), Denis Cheryshev (Urusi), Lazaros Christodoulopoulos (AEK Athens), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Giorgian de Arrascaeta (Cruzeiro), Riley McGree (Newcastle Jets), Lionel Messi (Argentina), Benjamin Pavard (Ufaransa), Ricardo Quaresma (Ureno), Mohamed Salah (Liverpool)

Tuzo ya nidhamu ya juu:

Shabiki wa mwaka: Sebastian Carrera (Puerto Montt), mashabiki wa Peru, Japan na Senegal

Wanasoka 11 bora (Fifa FIFPro World XI): Watachaguliwa kutoka kwa orodha ya wawaniaji 55. Orodha yenyewe hii hapa chini:

Makipa (5)

Gianluigi Buffon – Italia, Juventus/Paris Saint-Germain

Thibaut Courtois – Ubelgiji, Chelsea/Real Madrid

David De Gea – Uhispania, Manchester United

Keylor Navas – Costa Rica, Real Madrid

Marc-Andre ter Stegen – Ujerumani, Barcelona

Mabeki (20)

Jordi Alba – Uhispania, Barcelona

Dani Alves – Brazil, Paris Saint-Germain

Daniel Carvajal – Uhispania, Real Madrid

Giorgio Chiellini – Italia, Juventus

Virgil van Dijk – Uholanzi, Southampton/Liverpool

Diego Godin – Uruguay, Atletico Madrid

Mats Hummels – Ujerumani, Bayern Munich

Joshua Kimmich – Ujerumani, Bayern Munich

Dejan Lovren – Croatia, Liverpool

Marcelo – Brazil, Real Madrid

Yerry Mina – Colombia, Barcelona/Everton

Benjamin Pavard – Ufaransa, Stuttgart

Gerard Pique – Uhispania, Barcelona

Sergio Ramos – Uhispania, Real Madrid

Thiago Silva – Brazil, Paris Saint-Germain

Kieran Trippier – Uingereza, Tottenham Hotspur

Samuel Umtiti – Ufaransa, Barcelona

Raphael Varane – Ufaransa, Real Madrid

Sime Vrsaljko – Croatia, Atletico Madrid/Inter

Kyle Walker – Uingereza, Manchester City

Viungo (15)

Sergio Busquets – Uhispania, Barcelona

Casemiro – Brazil, Real Madrid

Philippe Coutinho – Brazil, Liverpool/Barcelona

Kevin De Bruyne – Ubelgiji, Manchester City

Eden Hazard – Ubelgiji, Chelsea

Andres Iniesta – Uhispania, Barcelona/Vissel Kobe

Isco – Uhispania, Real Madrid

N’Golo Kante – Ufaransa, Chelsea

Toni Kroos – Ujerumani, Real Madrid

Nemanja Matic – Serbia, Manchester United

Luka Modric – Croatia, Real Madrid

Paul Pogba – Ufaransa, Manchester United

Ivan Rakitic – Croatia, Barcelona

David Silva – Uhispania, Manchester City

Arturo Vidal – Chile, Bayern Munich/Barcelona

Washambuliaji (15)

Karim Benzema – Ufaransa, Real Madrid

Edinson Cavani – Uruguay, Paris Saint-Germain

Paulo Dybala – Argentina, Juventus

Antoine Griezmann – Ufaransa, Atletico Madrid

Harry Kane – Uingereza, Tottenham Hotspur

Robert Lewandowski – Poland, Bayern Munich

Romelu Lukaku – Ubelgiji, Manchester United

Mario Mandzukic – Croatia, Juventus

Sadio Mane – Senegal, Liverpool

Kylian Mbappe – Ufaransa, Paris Saint-Germain

Lionel Messi – Argentina, Barcelona

Neymar Junior – Brazil, Paris Saint-Germain

Cristiano Ronaldo – Ureno, Real Madrid/Juventus

Mohammed Salah – Misri, Liverpool

Luis Suarez – Uruguay, Barcelona 

You can share this post!

Wakazi wang’angania mahindi baada ya watu 4 kuangamia...

Matumaini ya Kawangware Utd kuhifadhi ubingwa yazimwa

adminleo