• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:53 PM
Wabunge waapa kupinga juhudi za kuhalalisha ushoga

Wabunge waapa kupinga juhudi za kuhalalisha ushoga

Na WINNIE ATIENO

WABUNGE wamesisitiza kuwa serikali ya Kenya haitaruhusu ushoga, usagaji wala ndoa za watu wa jinsia moja nchini.

Akiongea kwenye mkutano katika hoteli ya Serena Beach, Kaunti ya Mombasa, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu habari, mawasiliano na teknolojia Bw William Kisang, alisisitiza kuwa mapenzi ya jinsia moja ni haramu Kenya.

“Katiba iko bayana kuhusiana na masuala haya. Nyote mnajua mapenzi ya jinsia moja ni haramu na hatuhitaji sheria nyingine,” alisema Bw Kisang ambaye pia ni mbunge wa Marakwet Magharibi.

Kamati hiyo ilimpongeza mwenyekiti wa bodi ya kudhibiti filamu nchini Ezekiel Mutua katika harakati zake za kuhakikisha kuna maadili nchini hasa kwenye vipindi vinavyopeperushwa kupitia vyombo vya habari.

“Tunaunga juhudi za bodi ya kudhibiti filamu nchini katika kuhakikisha filamu za humu nchini zinafuata maadili ya jamii ya Kiafrika” akasema Bw Kisang.

Akizungumza katika mkutano huo, Dkt Mutua alisema filamu inayopigia upeto mapenzi ya jinsia moja inayojulikana kama Rafiki, haifai kuonyeshwa kuanzia leo.

Alisema yeyote atakayepatikana akionyesha filamu hiyo atachukuliwa hatua kwa kuvunja sharia.

Wiki iliyopita, mahakama kuu iliondoa kwa muda marufuku iliyowekwa na bodi ya Dkt Mutua ili ikubalike kwenye maonyesho ya Oscars.

You can share this post!

Gavana lawamani kuzima mashindano ya urembo

Mtoto wa miaka 2 anajisiwa, kunyongwa na kutupwa chooni

adminleo