• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 5:55 AM
Walimu wawili wauawa na Al Shabaab shuleni

Walimu wawili wauawa na Al Shabaab shuleni

 MANASE OTSIALO na CHARLES WASONGA

WALIMU wawili waliuawa Jumatano katika Shule ya Upili ya Wavulana ya Arabia, kaunti ya Mandera baada watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al – Shabaab kuvamia shule hiyo.

Kamishna wa kaunti ya Mandera Kutswa Olaka alithibitisha shambulio hilo kupitia taarifa akisema washambuliaji walirusha vilipuzi katika eneo la makazi ya walimu.

“Wavamizi hao wanaoaminika kuw wafuasi wa Al Shabaab walivamia makazi ya walimu katika Shule ya Upili ya Wavalana ya Arabia, iliyoko umbali wa kilomita moja kutoka mpaka wa Kenya na Somalia,” akasema.

Kulingana na Bw Kutswa, polisi wanne wa akiba ambao wamekuwa wakitoa ulinzi katika shule hiyo walilemewa na washambuliaji hao ambao hakutoa idadi yao.

“Kulikuwa na polisi wanne wa akia ambao walikuwa wakilinda shule hiyo wakati huo na wakilabiliana na wavamizi hao lakini kwa bahati wahuni hao waliwalemea na kisha wakatoweka, akasema.

Kambi ya polisi ya Arabia inapatikana umbali wa nusu kilomita kutoka shule hiyo. Maafisa wa polisi wa utawala wenye magari ya kivita pia wako katika kambi hiyo.

Afisa mmoja ambayo hakutaka kutajwa jina alisema kulikuwa na hali ya kukanganyikiwa miongoni mwa maafisa katika kambi hiyo wakati wa shambulio hilo kwani wengi wao walidhani kuwa polisi wa akiba shuleni humo walikuwa wakifanyia bunduki zao majaribio.

“Polisi hao wa akiba walikuwa wakifanyia majaribio bunduki zao mwendo wa saa nane za usiku na mlio huo ulisikika kama wa kawaida mwanzoni. Lakini baadaye tuligundua kuwa mlio huo wa risasi ulikuwa ni shambulio,” afisa huyo akasema.

Lakini kwenye taarifa yake Bw Kustwa alishikilia kuwa maafisa wa usalama walifika shule humo kwa haraka na wakakabiliana na washambuliaji hao.

“Maafisa wa usalama wanaendelea kuwasaka washambuliaji hao,” akaongeza.

Walimu wengine wasiotoka eneo hilo waliokuwa wakiishi katikia nyumba za karibu walifanikiwa kutorokea msitu kuokoa maisha yao.

Marehemu walitambuliwa kama Philip Okumu Masinde, 26 aliyehamishiwa shuleni humo mwaka jana na Daniel Wanjala aliyeanza kazi hapo 2016.

Mbw Elijah Nderitu na Kelvin Lomusi aliwaponea kwa tundu la sindano na wakahamishiwa mjini Mandera ambako kuna usalama.

Bw Kutswa alifeli kuelezea ni kwa nini walimu wasio wa asili ya eneo hilo bado walikuwa wakifunza katika shule zilizoko katika maeneo hatari ya mpaka wa Kenya na Somali, licha ya agizo la serikali kwamba wahamishiwe maeneo ya miji ambako kuna usalama wa kutosha.

You can share this post!

Kura ya maamuzi haiwezi kufanyika – Murkomen

Bunge latetea wanafunzi wa vyuo vya kiufundi

adminleo