• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 6:50 AM
Safaricom yapoteza wateja 470,000

Safaricom yapoteza wateja 470,000

Na BERNARDINE MUTANU

Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Safaricom inazidi kupoteza wateja huku washindani wake, Airtel, na Telcom wakiimarisha dadi yao ya wateja wapya.

Katika ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (CA) Safaricom inaendelea kutorosha wateja ingawa Airtel na Telkom zinaendelea kuvutia wateja.

Katika takwimu zilizotolewa wiki hii na CA, Airtel Kenya imepata wateja wapya milioni 3.56 katika muda wa mwaka mmoja uliopita.

Hii ni kumaanisha kuwa idadi ya wateja wapya iliongezeka kwa asilimia 50.61 hadi wateja 9.74 milioni katika mwaka wa kifedha uliokamilika Juni 2018.

Kwa upande wake, Telkom Kenya ilipata ongezeko la wateja wapya kwa asilimia 37.59 ambapo ilipata wateja milioni 1.09 wapya.

Hata hivyo, idadi ya wateja wapya wa Safaricom iliongezeka kwa asilimia 1.86 pekee (551,152) katika kipindi hicho.

Kufikia sasa Safaricom ina wateja 29.78 milioni. Kampuni hiyo ilipoteza uwezo wake kwa asilimia 7.2 hadi asilimia 65.35 katika kipindi cha mwaka mmoja, ilhali Airtel iliimarika sokoni kwa asilimia 6.02 na Telkom Kenya iliongeza uwezo wake sokoni kwa asilimia 8.76.

Safaricom ilipoteza wateja 470,000 katika muda huo.

You can share this post!

Sh15 bilioni za mradi wa vipakatalishi vya bure ziliyeyuka...

Mmiliki wa Zuku kuaga soko la Kenya

adminleo