• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 3:03 PM
Wachuuzi Wachina wamepokonya Wakenya ajira, watimuliwe – Wabunge

Wachuuzi Wachina wamepokonya Wakenya ajira, watimuliwe – Wabunge

Na BERNARDINE MUTANU

WABUNGE kumi sasa wanataka wachuuzi kutoka China, madereva na wahudumu wengine kutoka nchini humo kufukuzwa nchini kwa kutwaa kazi za Wakenya.

Wabunge hao kutoka Nairobi na Eneo la Kati wanataka leseni zote zilizotolewa kwa raia hao wa kigeni kufanya kazi nchini zinazoweza kufanywa na Wakenya kubatilishwa mara moja.

Wakiongozwa na mbunge wa Kiharu Dindi Nyoro, walimtaka Waziri wa Masuala ya Ndani Fred Matiang’i kutekeleza operesheni ya kuwanasa raia hao wa kigeni.

Walisema kuna ongezeko la raia wa China wanaochuuza au wana biashara ya rejareja nchini.

“Ingawa tunampongeza Dkt Matiang’i kwa operesheni dhidi ya wahamiaji haramu, tunamtaka kuanzisha tena zoezi hilo kwa sababu inaonekana wageni wote hawakuondoka. Wachina wamo kila mahali wakichuuza,” alisema.

“Kulikuwa na Mchina aliyeita rais tumbili, hatuwezi kukubali kuendelea kutusiwa,” alisema Mwakilishi wa Kike kutoka Laikipia Catherine Waruguru.

Alisema Wachina wana vibanda vya kuuza nguo katika soko la Gikomba, na wengine wanachoma mahindi.

You can share this post!

TAHARIRI: Wakati wa kuwalinda wanahabari ni sasa

TUZO ZA KPL 2018: Orodha nzima ya wachezaji watakaomenyana

adminleo