• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 8:55 AM
TUZO ZA KPL: Orodha nzima ya wachezaji waliojizolea hela

TUZO ZA KPL: Orodha nzima ya wachezaji waliojizolea hela

Na GEOFFREY ANENE

ERICK Kapaito alitia kibindoni Sh1,775, 000 katika msimu wake wa kwanza kabisa katika Ligi Kuu ya Soka ya Kenya baada ya kutangazwa Mwanasoka Bora wa mwaka 2018 pamoja na kuwa Mfungaji Bora na Mchezaji mpya wa mwaka katika hafla ya kufana jijini Nairobi, Oktoba 25, 2018.

Mshambuliaji huyu wa Kariobangi Sharks pia alimaliza kitengo cha Mchezaji mwenye nidhamu katika nafasi ya pili nyuma ya Mwanasoka bora wa mwaka 2017 Michael Madoya.

Katika tuzo hizo za mwaka 2018, taji la Kipa Bora, ambalo mchezaji mpya wa St Georges ya Ethiopia Patrick Matasi alishinda mwaka 2016 na 2017, lilinyakuliwa na Farouk Shikalo kutoka Bandari FC.

Shikalo alizawadiwa Sh500, 000 kwa kutofungwa bao katika mechi 18 kati ya 34 kwenye Ligi Kuu. Matasi, ambaye alijiunga na miamba hao wa Ethiopia hapo Oktoba 18 akitokea Tusker FC, aliridhika katika nafasi ya pili naye Kevin Omondi wa SoNy Sugar akafunga tatu-bora. Raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felly Mulumba kutoka Bandari FC aliibuka Beki bora wa mwaka, chipukizi Cliff Nyakeya wa Mathare United akashinda tuzo ya Kiungo bora wa mwaka, naye Madoya akaridhika na taji la Mchezaji aliyedumisha nidhamu ya hali ya juu.

Muingereza Dylan Kerr alitangazwa mshindi wa kitengo cha Kocha bora wa mwaka baada ya kuongoza Gor Mahia kutwaa taji la pili mfululizo na la 17 kwa jumla. Gor ndiyo klabu iliyokuwa na nidhamu ya juu ligini mwaka 2018. Tuzo hizi hudhaminiwa na kampuni ya bahati nasibu ya SportPesa, ambayo pia inadhamini Ligi Kuu.

Hii hapa orodha nzima ya washindi na zawadi wawaniaji walipata:

Mchezaji bora wa mwaka (MVP)

Eric Kapaito (Kariobangi Sharks) – mshindi (Sh1, 000, 000)

Michael Madoya (Zoo Kericho)

Farouk Shikalo (Bandari)

Cliff Nyakeya (Mathare United)

Felly Mulumba (Bandari/DR Congo)

Kipa bora wa mwaka

Farouk Shikalo (Bandari) – mshindi (Sh500, 000)

Patrick Matasi (Tusker) – nambari mbili (Sh300, 000)

Kelvin Omondi (SoNy Sugar) – nambari tatu (Sh200, 000)

Mathias Kigonya (Sofapaka/Uganda)

Ezekiel Owade (AFC Leopards)

Beki wa mwaka

Felly Mulumba (Bandari/DR Congo) – mshindi (Sh300, 000)

Titus Achesa (Posta Rangers) – nambari mbili (Sh200, 000)

Oliver Ruto (Ulinzi Stars) – nambari tatu (Sh100, 000)

Haron Shakava (Gor Mahia)

Joash Onyango (Gor Mahia)

Kiungo wa mwaka

Cliff Nyakeya (Mathare United) – mshindi (Sh300, 000)

Elvis Nandwa (Ulinzi Stars) – nambari mbili (Sh200, 000)

Michael Madoya (Zoo Kericho) – nambari tatu (Sh100, 000)

Marvin Nabwire (AFC Leopards)

Whyvonne Isuza (AFC Leopards)

Mchezaji mpya wa mwaka

Eric Kapaito (Kariobangi Sharks) – mshindi (Sh200, 000)

Marvin Nabwire (AFC Leopards) – nambari mbili (Sh75, 000)

Pistone Mutamba (Sofapaka) – nambari tatu (Sh50, 000)

Dennis Boge (Vihiga United)

Amos Kigadi (Vihiga United)

Mchezaji mwenye nidhamu

Michael Madoya (Zoo Kericho) – mshindi (Sh200, 000)

Eric Kapaito (Kariobangi Sharks) – nambari mbili (Sh75, 000)

Felly Mulumba (Bandari/DR Congo) – nambari tatu (Sh50, 000)

Pistone Mutamba (Sofapaka)

Dennis Boge (Vihiga United)

Kocha wa mwaka

Dylan Kerr (Gor Mahia/Uingereza) – mshindi (Sh300, 000)

Danstan Nyaudo (Ulinzi Stars) – nambari mbili (Sh175, 000)

John Baraza (Sofapaka) – nambari tatu (Sh50, 000)

Bernard Mwalala (Bandari)

Robert Matano (Tusker)

Meneja wa Timu wa mwaka

Vincent Okello (Mathare United) – mshindi (Sh100, 000)

Christopher Ouma (Ulinzi Stars) – nambari mbili (Sh75, 000)

Lazarus Yogo (Zoo Kericho) – nambari tatu (Sh50, 000)

Francis Onywera (Kariobangi Sharks)

Emmanuel Geno (Sony Sugar)

Mfungaji bora wa mwaka

Eric Kapaito (Kariobangi Sharks) – mshindi (Sh500, 000)

Elvis Rupia (Nzoia Sugar) – nambari mbili (Sh250, 000)

Jacques Tuyisenge (Gor Mahia) – nambari mbili (Sh250, 000)

Klabu ilioonyesha nidhamu ya hali ya juu

Gor Mahia – mshindi (Sh225, 000)

Sofapaka – nambari mbili (Sh175, 000)

Kariobangi Sharks – nambari tatu (Sh100, 000)

Refa wa kupuliza kipenga aliyeimarika zaidi

Davies Omweno (Makanika/Dereva wa lori) – mshindi (Sh200, 000)

Raymond Onyango (Afisa wa michezo) – nambari mbili (Sh75, 000)

Yasin Badr (Dereva) – nambari tatu (Sh50, 000)

Andrew Juma (Mwanahabari)

Israel Mpaima (Afisa wa masuala ya fedha)

Refa wa kunyanyua kibendera aliyeimarika zaidi

Gilbert Cheruiyot (mwalimu) – mshindi (Sh100, 000)

Maryann Njoroge (mfanyibishara) – nambari mbili (Sh75, 000)

Oliver Odhiambo (afisa wa kulinda wanyama pori) nambari tatu (Sh50, 000)

Tonny Kidiya (mwalimu)

Stephen Yembe (Mtaalamu wa masuala ya kidijitali)

Zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Ligi Kuu (KPL):

GMT Ottieno – Sh100, 000

You can share this post!

DIMBA PATRIOTS: Vipaji vya soka mtaani Kangemi

Nitafuata masharti yote – Obado

adminleo