• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:40 AM
Mtahiniwa wa KCSE aanguka  na kufariki

Mtahiniwa wa KCSE aanguka na kufariki

Na NDUNGU GACHANE

MTAHINIWA wa Kidato cha Nne (KCSE) wa Shule ya upili ya Gaichanjiru Boys alianguka ghafla na kufariki Jumapili wakati wa shoo ya burudani shuleni humo.

Hata hivyo, wazazi wake wanashauku na kilichosababisha kifo chake na wanataka uchunguzi wa kina ufanywe kubaini kilichojiri.

Kulingana na Kamanda wa polisi kaunti ya Murang’a, Bw Mohammed Farah, wasimamizi wa shule waliwafahamisha kuwa, mwanafunzi Roy Ngahu alianguka akisakata ngoma wakati wa kipindi cha burudani. Mwanafunzi huyo alithibitishwa kufariki baada ya kufikishwa katika hospitali ya misheni ya Gaichanjiru.

Bw Farah alisema wanasubiri ripoti ya upasuaji maiti ingawaje uchunguzi wa awali ulionyesha kuwa alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.

Mkurugenzi wa elimu kaunti, Victoria Mulili alisema watafuatilia ripoti ya uchunguzi wa maiti kabla ya kutoa kauli yao.

post-mortem kabla hawajatoa kauli zaidi kuhusu kufariki kwa mtahiniwa huyo.

Hata hivyo babake marehemu, Daniel Ngahu anashuku kuna jambo linalofichwa na uongozi wa shule hiyo kuhusu kifo cha mtoto wake haswa baada kushawishiwa na kushinikizwa kuharakisha mchakato mzima wa kuondoa mwili kutoka hifadhi ya maiti ya Gaichanjiru karibu na shule hiyo. .

“Sielewi kwa nini usimamizi wa shule ulikuwa mwepesi wa kunishinikiza kuondoa mwili kutoka hifadhi hiyo karibu na shule na hata kuwa tayari kugharamia usafiri wake hadi hifadhi nyingine huku wakinihakikishia wangefuatilia suala hilo baadaye,” akasema Bw Ngahu.

You can share this post!

TAHARIRI: Ni aibu kwa waziri kutoheshimu hadhi

Juhudi za kuwapatanisha Echesa na Malala zaanza

adminleo