• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Bondia aliyemuua kocha wake asukumwa jela miaka 20

Bondia aliyemuua kocha wake asukumwa jela miaka 20

Na BRIAN OCHARO

BONDIA aliyemuua kocha wake miaka mitano iliyopita baada ya kutokubaliana juu ya mafunzo amefungwa jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.

Yonah Onyango alihukumiwa baada ya mahakama kuamua kwamba alimwua kocha wake kulipiza kisasi dhidi yake.

“Ninaona kwamba mashtaka imeonyesha akiwa na nia ya kumdhuru Mohamed Salim na alimdhuru mbele ya shahidi,” Jaji Asenath Ongeri alisema

Hakimu huyo alisema kuwa ilikuwa dhahiri kwamba mtuhumiwa alikuwa na sababu mbaya ya kulipiza kisasi dhidi ya kocha wake ambaye walipigana naye kwenye mazoezi kabla ya mauaji.

“Upande wa Mashtaka umethibitisha kesi yake kwa kiwango kinachohitajika na mahakama inahukumu mtuhumiwa kama alivyoshtakiwa , ingawa mtuhumiwa anawajibika, anahukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani ,” hakimu alisema.

Mshukiwa huyo mwenye umri wa miaka 24 alikuwa ameiambia mahakama kuwa marehemu huyo alikuwa akimdharau na kuwa alimuua kibahati mbaya akiwa anajitetea.

Bw Onyango aliiambia mahakama kuwa alikuwa akijitetea dhidi ya kocha wake ambaye alimvamia akiwa na panga.

Anashutumiwa kumuua Bw Salim mnamo Oktoba 4, 2013 katika eneo la Mtongwe huko Likoni.

Mahakama hiyo iliambiwa kuwa mtuhumiwa ambaye alifanya kazi ya kuendesha mkokoteni alianzishwa kwenye mchezo huo ambapo alikuwa akifundishwa na Salim.

Kiongozi wa Mashtaka Ngina Mutua alisema kuwa siku ya tukio, mtuhumiwa alimwambia marehemu kuwa alikuwa amechoka kwa kuchaguliwa wakati wote kupigana na wenzake lakini hakutaka kusikiliza.

Pia, aliambia mahakama kuwa mara nyingi, kocha wake alikuwa akimnyima nafasi ya kufanya mazoezi , jambo ambalo lilikuwa likimkera.

Lakini kocha alisisitiza kwamba lazima apigane lakini hakuwa akipewa nafasi ya kufanya mazoezi , mshukiwa huyo alikasirika na vita vikaanzia katika ukumbi ya kufanyia mazoezi.

Wawili hao waliamuliwa baada ya mapigano makali lakini mshtakiwa aliendelea na chuki ndani yake na kumfuata kocha kwa nyumba yake jioni ya siku hiyo.

Kwa mujibu wa Bi Mutua, mtuhumiwa baadaye alishambulia kocha ambaye alikuwa jirani yake katika makao yake na vita vilifuata.

Ni wakati huu ndio mshukiwa alimdunga mwendazake kisu ya tumbo kwa kumdharao na kumnyima nafasi ya kufanya mazoezi huku akihitajika kupigana na wenzake.

Bw Onyango alijitetea akisema kuwa mwendazake alishambulia kwa panga kabla ya mapigano kutokea kati yao.

“Mwendazake alinishambulia na ilikuwa ni haki yangu kujikinga,” alisema.

Mtuhumiwa alisema kwa njia ya mwanasheria wake kwamba mashahidi wote upande wa mashtaka walisema kulikuwa na mapambano kati yake na Bw Salim.

Alisisitiza kuwa alijikinga dhidi ya marehemu lakini kwa bahati mbaya tukio hilo lilisababisha kifo cha Bw Salim.

“Ninahimiza mahakama kutilia maanani utetezi wangu kuwa nilikuwa nikijikinga dhidi ya marehemu, sikuwa na nia fiche,” alisema.

Mtuhumiwa huyo alielezea kuwa marehemu alikuwa rafiki wake mkubwa na kuongezea kuwa hakuwa na sababau yoyote ya kumuua, aliongezea kuwa ni uchochezi uliosababisha vita na kifo cha marehemu.

“Si Kweli kwamba mshukiwa alivamiwa na marehemu, hata kama alivamiwa , mshukiwa angepiga ripoti kwa polisi. Madai hayo ni ya uongo na hayawezi kuzingatiwa,” Jaji Ongeri alisema.

  • Tags

You can share this post!

Wanakijiji 300 wakesha kwa kijibaridi kufuatia mzozo wa...

KPA, Mkuu wa Sheria wapinga kaunti isimamie bandari ya...

adminleo