• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Waliogura shule kuwa wanabodaboda wajitokeza ghafla kufanya KCPE

Waliogura shule kuwa wanabodaboda wajitokeza ghafla kufanya KCPE

GERALD BWISA na PETER MBURU

WANAFUNZI wanane wa Darasa la Nane katika Kaunti ya Trans Nzoia na ambao walikuwa wamegura masomo mapema mwaka huu baada ya kujisajili walijitokeza ghafla tena Jumanne kufanya mtihani wa KCPE, kisa kilichowaduwaza walimu na wanafunzi

Kulingana na mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Trans Nzoia Malea Agona, sita kati ya wanafunzi hao ambao ni wavulana walienda kuajiriwa vibarua kama waendeshaji wa boda boda, ilhali wasichana wawili waliolewa.

“Walifika shuleni wakati wa maandalizi Jumatatu na kama usimamizi wa shule tuliwaruhusu kufanya mitihani ambayo imeanza leo,” Be Agona akasema.

Hata hivyo, alisema kuwa wanafunzi wote waliosajiliwa shuleni humo ni 160 na kuwa ni mmoja tu ambaye hakufika kufanya mitihani wala hakutoa sababu yoyote.

Watahiniwa hao wanajumuisha watu wazima ambao walijisajili kwa mitihani wa mwaka huu.

Jumla ya watahiniwa 105 watu wazima wanafanya mitihani wa KCPE kaunti ya Trans Nzoia, huku Mzee zaidi akiwa na miaka 52.

Mkurugenzi wa elimu ya watu wazima eneo LA Trans Nzoia Magharibi Priscilla Rono aliewma kuwa watu wazima wanaofanya mtihani wako na matumaini ya kufanya vyema.

“Serikali imetoa fursa kwa watu ambao hawakufanya vyema ama ambao hawakusoma kwa mtaala wa sasa kuendeleza elimu kupitia elimu ya watu wazima,” Bi Rono akasema.

Jumla ya watahiniwa 26, 741 watafanya mtihani wa KCPE Kaunti ya Trans Nzoia mwaka huu katika vituo 539, wavulana wakiwa 13,415 na wasichana 13, 326.

Mtihani wa KCSE utakaliwa na watahiniwa 15,888, katika vituo 247.

You can share this post!

Baba na wanawe wawili kunyongwa kwa kumuua mvulana mchungaji

Serikali yajiandaa kukopa mabilioni tena

adminleo