• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
TAHARIRI: Wanaopachika watoto mimba wakabiliwe vikali

NA MHARIRI

VISA vya wasichana wachanga kupata mimba wakiwa wangali shuleni ni ishara ya jamii ambayo imeshindwa kuwalinda watoto wa kike dhidi ya wanaume wasio na maadili.

Hapo jana kuliripotiwa visa vya wasichana kadhaa kujifungua wakati wakifanya mtihani wa KCPE. Ripoti za wasichana wa shule za msingi kupata mimba pia ziko nyingi katika sehemu mbalimbali za nchi.

Sababu za wasichana hawa kujipata mikononi mwa wanaume wanaowadanganya kushiriki mapenzi wakiwa wachanga ni nyingi.

Kumekuwa kukiripotiwa kuwa umaskini unachangia katika wengi wao kushawishika kushiriki ngono na wanaume wanaowaahidi kuwapa pesa za kununua sodo, chakula, nguo miongoni mwa ahadi zingine.

Wasichana hawa ni watoto ambao hujipata katika hali ya kushawishika, na mchango wao katika hali ambazo zinawafanya kushika mimba unakuwa mdogo kwani hawafahamu matokeo ya kitendo hicho na pia kutokana na umri wao hawana uwezo wa kukataa wanayoambiwa.

Jamii ndiyo ya kulaumiwa kwa kutatiza maisha ya watoto wa kike wanaobebeshwa mimba. Hali hii inaonyesha jamii yenye wanaume ambao wanaongozwa na hisia za kimwili badala ya kutumia akili. Hii ni hasa pale mimba hizi zinakuwa ni za wanaume waliokomaa.

Jamii yoyote ile inafaa kuwalinda watoto kwa kuwaona kama watoto wala sio viumbe vya kushiriki ngono navyo.

Wanaume wanaowatia wasichana wadogo mimba huwa wamekosa ule ubinadamu wa kuwaona wasichana wachanga kama watoto na badala yake wanaongozwa na hisia zinazowasukuma kushiriki mapenzi na watoto hao.

Kutokana na wingi wa visa hivi, maafisa wa utawala pamoja na jamii yote kwa jumla wanafaa kushirikiana katika kuhakikisha kuwa wanaohusika katika kuwapachika mimba watotob wamekamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Hawa wanapasa kufunguliwa mashtaka kama vile unajisi kutokana na ukweli kuwa mtoto hana uwezo wa kuamua kushiriki ngono kwa hiari yake mwenyewe.

Hatua hizi za kisheria zitasaidia kuzima wale ambao wanawamezea mate wasichana wachanga na kuharibu mwelekeo wao wa kimaisha.VISA vya wasichana wachanga kupata mimba wakiwa wangali shuleni ni ishara ya jamii ambayo imeshindwa kuwalinda watoto wa kike dhidi ya wanaume wasio na maadili.

Hapo jana kuliripotiwa visa vya wasichana kadhaa kujifungua wakati wakifanya mtihani wa KCPE. Ripoti za wasichana wa shule za msingi kupata mimba pia ziko nyingi katika sehemu mbalimbali za nchi.

Sababu za wasichana hawa kujipata mikononi mwa wanaume wanaowadanganya kushiriki mapenzi wakiwa wachanga ni nyingi.

Kumekuwa kukiripotiwa kuwa umaskini unachangia katika wengi wao kushawishika kushiriki ngono na wanaume wanaowaahidi kuwapa pesa za kununua sodo, chakula, nguo miongoni mwa ahadi zingine.

Wasichana hawa ni watoto ambao hujipata katika hali ya kushawishika, na mchango wao katika hali ambazo zinawafanya kushika mimba unakuwa mdogo kwani hawafahamu matokeo ya kitendo hicho na pia kutokana na umri wao hawana uwezo wa kukataa wanayoambiwa.

Jamii ndiyo ya kulaumiwa kwa kutatiza maisha ya watoto wa kike wanaobebeshwa mimba. Hali hii inaonyesha jamii yenye wanaume ambao wanaongozwa na hisia za kimwili badala ya kutumia akili. Hii ni hasa pale mimba hizi zinakuwa ni za wanaume waliokomaa.

Jamii yoyote ile inafaa kuwalinda watoto kwa kuwaona kama watoto wala sio viumbe vya kushiriki ngono navyo.

Wanaume wanaowatia wasichana wadogo mimba huwa wamekosa ule ubinadamu wa kuwaona wasichana wachanga kama watoto na badala yake wanaongozwa na hisia zinazowasukuma kushiriki mapenzi na watoto hao.

Kutokana na wingi wa visa hivi, maafisa wa utawala pamoja na jamii yote kwa jumla wanafaa kushirikiana katika kuhakikisha kuwa wanaohusika katika kuwapachika mimba watotob wamekamatwa na kushtakiwa kwa mujibu wa sheria.

Hawa wanapasa kufunguliwa mashtaka kama vile unajisi kutokana na ukweli kuwa mtoto hana uwezo wa kuamua kushiriki ngono kwa hiari yake mwenyewe.

Hatua hizi za kisheria zitasaidia kuzima wale ambao wanawamezea mate wasichana wachanga na kuharibu mwelekeo wao wa kimaisha.

You can share this post!

Gharama ya kuendesha magereza kupunguzwa

WANDERI: Waafrika wanachangia ukoloni-mamboleo

adminleo