• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 10:55 AM
Bayern yaomba kuandaa fainali ya UEFA 2021

Bayern yaomba kuandaa fainali ya UEFA 2021

Na CECIL ODONGO

KLABU ya Bayern Munich imewasilisha ombi ikitaka kuwa mwenyeji wa  fainali ya klabu bingwa barani Uropa mwaka wa 2021.

“Naweza kuthibitisha kwamba Bayern, pamoja na mji wa Munich itatuma ombi rasmi la kuwa mwenyeji wa fainali ya klabu bingwa barani Uropa mwaka wa 2021 kwenye uga wa  Allianz Arena,” akasema Afisa Mkuu Mtendaji wa Bayern Munich Karl-Heinz Rummenigge.

Bayern iliandaa fainali ya mwaka wa 2012 lakini ikaaibishwa na Chelsea kupitia mikwaju ya penalti na taji hilo kuwaponyoka nyumbani kwao huku huzuni ambao haujawahi kushuhudiwa Ujerumani ikitandaa katika mji wa Munich.

“Ingawa tulitamaushwa kwa kushindwa na Chelsea mwaka wa 2012 bado tunaenzi kumbukumbu ya kuiandaa fainali hiyo nyumbani. Tutakuwa wingi wa shukrani iwapo shirikisho la soka barani ulaya UEFA litatupa nafasi ya kuukaribisha umma wa soka mjini Munich kwa mara nyingine,” akaongeza Karl-Heinz Rummenigge.

Hata hivyo Bayern itapokea ushindani mkali kutoka kwa uga wa Krestovsky nchini Urusi ambao unamilikiwa na klabu ya  Zenit St. Petersburg iliyoonyesha nia ya kuwa mwenyeji wa kipute hicho mwaka huo wa 2021.

Seville, Vienna na Tbilisi ndizo nyuga pekee zilizotuma maombi ya kuandaa fainali ya ligi ya Uropa mwaka wa 2021 huku nyanja za Belfast, Kharkiv, Minsk na Helsinki zikiwania nafasi ya kuwa mwenyeji wa UEFA Super Cup.

Nyuga za Gothenburg na Prague zinatumai kwamba moja yazo itateuliwa kuandaa faina ya ligi ya klabu bingwa barani Uropa ya wanawake (Women’s Champions League).

  • Tags

You can share this post!

Mahrez anusia tuzo ya mchezaji bora kikosini Man City

Wamiliki wa biashara ndogo hawatasazwa na KRA

adminleo