• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 10:08 PM
SHERIA ZA MICHUKI: Wenye matatu walivyogharimika kutii sheria

SHERIA ZA MICHUKI: Wenye matatu walivyogharimika kutii sheria

Na BERNARDINE MUTANU

Wamiliki wa magari ya uchukuzi wa umma Jumanne walilazimika kutoa kati ya Sh30, 000 na Sh100, 000 kwa lengo la kutekeleza kanuni za trafiki.

Baadhi yao walipata hasara kubwa kwa kuamua kuondoa magari yao barabarani kwa kuhofia kukamatwa.

Mawaziri wa Uchukuzi na Usalama wa Ndani James Macharia na Fred Matiang’i mtawalia wametangaza utekelezaji upya wa sheria za trafiki.

Kulingana na sheria hizo mpya, magari yote yanafaa kuwekwa mishipi vitini, vidhibiti mwendo vipya, bima na leseni.

Kulingana na sheria hizo, magari ya uchukuzi wa umma yanaweza kutozwa kati ya Sh1, 000 na Sh10, 000 kwa kukataa kutekeleza sheria hizo.

Tayari mashirika husika ya wizara hizo mbili yakiwemo Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA), idara ya polisi na Mwendeshaji wa Mashtaka ya Umma (DPP) yameanzisha operesheni kuhakikisha kuwa magari ya uchukuzi wa umma yanatekeleza sheria za trafiki.

Kufikia Jumanne, Inspekta Mkuu wa Polisi Joseph Boinnet alitangaza kubatilishwa jwa vyama 64 vya matatu na kukamatwa kwa madereva na makanga 2,000 kwa kukataa kutekeleza kanuni mpya.

You can share this post!

Wakenya 13 waomba kazi ya kusimamia EACC

TEKNOLOJIA: Mtangazaji wa kwanza roboti duniani mmakinifu...

adminleo