• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 8:55 PM
Aliyenoa kucha za Ingwe awazia kutua Gor

Aliyenoa kucha za Ingwe awazia kutua Gor

Na CECIL ODONGO

KOCHA wa zamani wa AFC Leopards Luc Eymael ni miongoni mwa wakufunzi wanaotajwa sana kama watakorithi mkoba wa ukufunzi wa Gor Mahia baada ya Dylan Kerr kujiuzulu Alhamisi Oktoba 15, 2018.

Eymael aliwanoa Ingwe mwaka wa 2013 kabla ya kukosana na uongozi wa klabu na kuendea zake. Kwa sasa ni kocha mkuu wa Free States Stars inayoshiriki ligi ya  Afrika Kusini, ABSA.

Gor Mahia pia wanasemekana wanatafuta huduma za kocha maarufu raia wa Brazil Roberto Oliveira.

Mkufunzi huyo aliye na miaka 52, ni kocha wa Rayon Sports ya Rwanda na alikuwa kwenye benchi yao ya kiufundi  jijini Nairobu wakati wa mechi ya Kombe la Mashirikisho msimu uliopita/2017-19, timu yake ilipowakalifisha K’Ogalo kwa mabao 2-1.

Hata hivyo duru za kuaminika  kutoka mabingwa hao mara 17 wa KPL zimearifu kwamba hakuna chochote kilichoafikiwa hadi sasa kuhusu uteuzi wa kocha mpya.

“Majina hayo yametajwa ila hakuna chochote kilichoafikiwa. Kutaandaliwa mikutano ya kuyajadili hayo na tutampa kandarasi tu mtu aliye na rekodi ya kuimarisha matokeo ya timu,” ikaarifu duru hizo.

K’Ogalo wana kibarua kigumu dhdi ya Nyasa Big Bullets  kutoka Malawi Novemba 27, 2018 kwenye mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi  ya klabu bingwa barani Afrika na pia kutetea taji lao la KPL msimu mpya uking’oa nanga mwezi Disemba.

  • Tags

You can share this post!

Matibabu ya figo yaanza Lamu

JAMAL KHASHOGGI: Mahakama yajiandaa kunyonga washukiwa...

adminleo