• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Dereva wa Umoinner amuua mwanabodaboda na kuingia mitini

Dereva wa Umoinner amuua mwanabodaboda na kuingia mitini

Na RICHARD MUNGUTI

HALAIKI kubwa ya watu ilikusanyika Ijumaa asubuhi katika steji ya Donholm  katika barabara ya Jogoo kumtazama mwanabodaboda aliyegongwa na basi la sacco ya Umoiner na kufa papo hapo.

Na wakati huo huo dereva wa matatu hiyo alitoroka mbio kwa miguu na kuiacha matatu hiyo katikati ya  barabara.

“Dereva huyooo anatoroka,”  afisa wa polisi wa trafiki alionyeshwa dereva huyo akitorokea katika mtaa wa Tena karibu na kituo cha petroli cha Shell kilichoko katika barabara  Outering karibu na mzunguko wa Donholm.

Ajali hiyo ilitokea mwendo was aa mbili asubuhi wakati mwendazake alijaribu kuipita basi hilo ya abiria 29 upande wa kulia.

Dereva wa basi hilo aliyekuwa anaendesha kwa kasi aliielekeza upande wa mwendeshaji pikipiki huyo. ‘Kile kilisikika ni mlipuko mkubwa.

Kufumba na kufumbua mwendeshaji huyo wa pikipiki huyo alianguka kwa kishindo katikati ya barabara na kupasuka kichwa na kuacha damu ikitapakaa kwenye barabara.

Gari hilo lilivuruta pikipiki hiyo ya marehemu umbali wa mita 10.

Ajali hiyo ilitokea wakati maafisa wa polisi wa trafiki walikuwa wakisaka magari ambayo hayajatimiza masharti ya sheria za trafik almaarufu Sheria za Michuki.

Watu waliokuwa wakielekea jiji la Nairobi, Embakasi, Kayole , Njiru na Viwandani walikongamana mahali hapo pa ajali kuishuhudia.

“Dereva huyu wa matatu hii ya Umoinner hakuwa mwangalifu,” akasema afisa mmoja wa polisi.

You can share this post!

KCSE: Mtahiniwa ajinyonga baada ya kufanya mtihani wa...

Polisi wang’oa bangi ya Sh15 milioni Migori

adminleo