• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 5:39 PM
KCSE:  Walimu 5, wanafunzi 18 wafikishwa mahakamani kuhusiana na wizi

KCSE: Walimu 5, wanafunzi 18 wafikishwa mahakamani kuhusiana na wizi

Na Jadson Gichana

WANAFUNZI 18 na walimu watano walifikishwa katika mahakama ya Ogembo kwa kosa la kupatikana na maswali ya mtihani wa KCSE.

Washukiwa hao ni watahiniwa katika wa shule ya Upili ya wavulana ya Nduru iliyoko, Kaunti Ndogo ya Gucha Kusini, Kaunti ya Kisii na walimu kutoka shule tofauti ambao walikuwa wanasimamia mtihani huo.

Walifikishwa mbele ya Hakimu Mkaazi, Bw Julius Mutai walikabiliwa na mashtaka mawili ya kupatikana na karatasi la mtihani.

Watahiniwa hao walishtakiwa kwa kupatikana na karatasi ya KCSE 311/1 la Historia ambalo lilikuwa limeandikwa ndani ya darasa mtihani huo ukiendelea Novemba 19, 2018 katika shule ya Nduru, Kaunti ya Kisii kinyume cha sheria.

Katika shtaka la pili Tom Osoro Reuben, Daniel Okiagera Mwangi, Evans Arumba Obare, Denis Ogake Nyaundi na Peter Nyandega Moenga walidaiwa mnamo Novemba 19 katika shule ya Upili ya wavulana ya Nduru Kaunti ndogo ya Gucha Kusini, Kaunti ya Kisii wakiwa wasimamizi katika kituo hicho cha mtihani, walikosa kuwakagua watahiniwa ambao walipatikana na vifaa vilivyoandikwa kwa mkono ndani ya kituo hicho.

walipatikana wakiwa wanamiliki karatasi hilo la mtihani wa Historia kinyume na sheria za Baraza la mtihani nchini (KNEC) 2012 katika kipengele 27(3).

Watasomewa mashtaka Desemba 5, 2018.

You can share this post!

KCPE: Siri ya kuwa juu miaka 10

KCPE: Shule ya Msingi ya Ikombe yaibuka bingwa kitaifa

adminleo