• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
DPP aishangaa mahakama kumwachilia huru Obado

DPP aishangaa mahakama kumwachilia huru Obado

Na PETER MBURU

KIONGOZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji ameeleza kughadhabishwa kwake na namna mahakama za humu nchini zimekuwa zikishughulikia kesi zinazowahusu watu wenye umaarufu.

Bw Haji alieleza kuwa mahakama zinawapendelea watu hao, ambao wengi wanahusisha maafisa wakuu katika serikali na ambao wamehusishwa na makossa makubwa ya jinai nay a kiuchumi.

Akirejelea kisa cha kesi zinazomkumba Gavana wa Migori Okoth Obado, DPP amesema kuwa ikilinganishwa na makosa mengi anayokumbana nayo gavana huyo na uzito wake, hakufaa kupewa dhamana.

Gavana Obado anakumbana na kesi tatu; ya mauaji, umiliki wa bunduki kinyume na sheria na ufisadi katika serikali ya kaunti ya Migori.

Bw Haji ameshangaa sababu ya mahakama kuruhusu maafisa wa utumishi wa umma kuendelea kufanya kazi, wakati wanakumbana na makossa makubwa akitaja hali hiyo kuwa iliyonyima taifa hadhi.

“Tumepeleka kesi kortini na kuwashtaki watu, wawe magavana, wamiliki wa afisi nyingine za kikatiba n ahata naibu wa Jaji Mkuu mwenyewe, lakini wengi wao bado wanasalia ofisini. Na pia kuna amri za korti zinazowaruhusu kufurahia uhuru wote,” Bw Haji akasema Jumanne.

Alitaja mazingira ambayo Gavana Obado alipewa dhamana kwa kesi ya mauaji kuwa ya kutatanisha.

“Mlimwona akifanya kazi na washirika wa maendeleo na huyu ni mtu anayekumbana na mashtaka ya mauaji, mtu ambaye amepatikana na bunduki ambazo hawezi kueleza kuzihusu katika nyumba yake,” akasema DPP.

Alisema kuwa sheria inasema maafisa wa umma ambao wanakumbana na mashtaka ya kutenda hatia kortini wajiuzulu hadi pale kesi zinapokamilika na ukweli kufahamika.

“Kuna suala kuwa mtu anachukuliwa kuwa hana kosa hadi korti itakapodhibitisha na kuwa maafisa wa umma wanafaa kujiuzulu hadi kesi inapokamilika na kutatuliwa. Hii ni sheria na tumejaribu kuzifanya mahakama kuelewa lakini bado washukiwa wanaruhusiwa kurejea ofisini na kuharibu ushahidi,” akasema.

DPP sasa anasema kuwa ataiandikia bunge kubadili sheria ili kila anaposhtakiwa afisa wa utumishi wa umma awe anajiuziulu hadi kesi ikamilike.

Gavana Obado aliachiliwa kwa mara ya kwanza kwa bondi ya Sh5milioni katika kesi yake kuhusiana na mauaji ya mwanafunzi wa chuo kikuu Sharon Otieno. Wiki iliyopita, gavana huyo alikamatwa tena kwa kesi ya umiliki wa bunduki, lakini tena akaachiliwa kwa dhamana.

You can share this post!

KCPE: Tohara inavyowazuia waliong’aa kusherehekea...

#MheshimiwaFisi: Wabunge wapapurwa mitandaoni kujaribu...

adminleo