• Nairobi
  • Last Updated April 24th, 2024 4:50 PM
Amuua baba mkwe kwa kukosa kurudisha ng’ombe wa mahari

Amuua baba mkwe kwa kukosa kurudisha ng’ombe wa mahari

Na PETER MBURU

MAHAKAMA Kuu imemwachilia mwanaume aliyedaiwa kumuua baba mkwe wake, baada yake kukataa kurejesha ngombe ambao mshukiwa alikuwa amelipa kama mahari, baada ya polisi kukosa ushahidi.

Bw Lekini Lepukuny alishtakiwa kuwa alimpiga na kumuua mzee Resipo Lesipia mnamo Desemba 2016 katika eneo la Posta, Makadara, Laikipia Kaskazini.

Hata hivyo, wakati kesi yake ilipokamilika Jumanne, mahakama ilimwondolea lawama na kumwachilia, baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha kwa viwango vifaavyo kuwa alitekeleza mauaji hayo.

Akimwachilia huru, Jaji Mary Kasango alisema mshukiwa hakuwa na kosa la mauaji namna alivyoshtakiwa.

Korti ilisikia kuwa mzozo uliibuka baada ya mshukiwa kudai ngombe wake kutoka kwa familia ya mkewe, japo babake mke wake alikuwa akidai wafanye mazungumzo kuhusu mzozo uliokuwepo.

Baadaye mshukiwa nadaiwa kujihusisha na fujo na wakwe zake, ambazo zilipelekea kifo cha baba mkwewe.

Lakini Jaji Kasango alisema kuwa kulingana na ushahidi uliotolewa mbele ya korti, mshukiwa alikuwa akijikinga, wala hakufanya mauaji ya moja kwa moja alipomgonga marehemu.

“Vita baina ya mshukiwa na marehemu huenda vilichangiwa na hali kuwa marehemu hakutaka ngombe wake kuchukuliwa,” jaji huyo akasema akitoa uamuzi.

  • Tags

You can share this post!

Wazee waitaka NACADA kutuma kikosi kuzima uraibu wa...

Murkomen na Kutuny wapakana tope mitandaoni

adminleo