• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 12:26 PM
Joho kuwaajiri waliopata ‘first class’ Chuo Kikuu cha Kiufundi, Mombasa

Joho kuwaajiri waliopata ‘first class’ Chuo Kikuu cha Kiufundi, Mombasa

Na DIANA MUTHEU

GAVANA wa Mombasa Hassan Joho Jumatano aliahidi kwamba serikali yake itawapa ajira mahafala walioibuka kidedea na kufuzu kwa shahada mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Mombasa (TUM).

Bw Joho alitoa ahadi hiyo wakati wa sherehe za sita za kufuzu kwa chuo hicho zilizoandaliwa kwenye bewa lake kuu la Tudor.

Jumla ya mahafali 2,316 walitunukiwa shahada mbalimbali baada ya kukamilisha masomo yao.

Hata hivyo, gavana huyo alikiomba chuo hicho kujikita katika kutoa mafunzo ya kozi zinazohitajika kwenye utoaji huduma kwa kaunti hiyo na zile zinazolenga kuhakikisha wanatumia ujuzi walioupata kuendeleza kaunti kwa kutimia rasilimali na maliasili iliyopo katika kaunti.

“Naomba tuanzishe kozi zitakotusaidia sisi binafsi na kaunti yetu. Lazima tufanye uamuzi wa busara utakaotusaidia katika utafiti. Tugeuze Hospitali Kuu ya Mkoa wa Pwani hadi Hospitali ya Rufaa na Mafunzo. Natumai wakati wa kufuzu ya 12 tutakuwa tunawasheherekea madaktari kutoka TUM,” akasema Bw Joho.

Kwa upande wake, Naibu Chansela wa chuo hicho Leila Abubakar aliwapa pongezi mahafala wote na kuwataka kutumia ujuzi waliopata kufanya biashara na kubuni nafasi zaidi za ajira.

“Tumieni ujuzi mlioupata kupata suluhisho kwa matatizo yanayoizonga nchi kama umaskini mkubwa miongoni mwa raia,” akatanguliza.

“Tunatumai kwamba ujuzi kutoka chuo hiki utawasaidia kuyainua maisha yenu na kuchangia vilivyo maendeleo ya kaunti na ya taifa zima,” akasema Prof Abubakar.

Huku akitaja kwamba idadi ya mahafali imeongezeka ikilinganishwa na miaka ya nyuma, Prof Leila alifichua kwamba Sh200 milioni zimetengwa kugharimia ujenzi wa bweni katika bewa ambalo litakidhi idadi ya wanafunzi 400 katika Kaunti ya Kwale ambalo.

Kulingana naye, kituo cha polisi pia kitajengwa karibu na bewa hilo ili kuwahakikishia wanafunzi usalama wao.

You can share this post!

Wanahabari huru kuangazia kesi ya ufisadi inayokabili Kenya...

Tamaduni za Wamakonde sasa kuhifadhiwa Bomas

adminleo