• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 3:17 PM
Nimetii masharti yote ya mahakama, asema Obado

Nimetii masharti yote ya mahakama, asema Obado

Na RICHARD MUNGUTI

GAVANA wa Migori Okoth Obado anayekabiliwa na shtaka la kumuua aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo Sharon Beryl Otieno na mwanawe Alhamisi aliambia mahakama kuu ametii masharti aliyopewa alipoachiliwa kwa dhamana Oktoba mwaka huu ya Sh5milioni pesa taslimu.

Kupitia kwa mawakili wake , Mabw Cliff Ombeta na Roger Sagana , Bw Obado alimweleza naibu wa msajili wa mahakama kuu Bi Roselyn Oganyo kuwa “hajakaidi agizo asisafiri umbali wa kilomita 20 nje ya kaunti ya Migori.”

Bw Ombeta alisema , gavana huyo anayeshtakiwa pamoja na aliyekuwa msaidizi wake Michael Oyamo na aliyekuwa katibu mkuu Bw Caspal Obiero, amekuwa mtiifu.

“Mshtakiwa amedumisha masharti aliyoamriwa na Jaji Jessie Lesiit alipomwachilia kwa dhamana,”alisema Bw Ombeta.

Mahakama ilifahamishwa kuwa Bw Obado ameendelea kuhudumia wakazi wa kaunti ya Migori na “kamwe hajawavuruga mashahidi.”

Washtakiwa hao walikana mnamo Septemba 4 , 2018 katika eneo la Homa Bay walimuua Sharon wakishirikiana na watu wengine ambao hawajakamatwa.

Gavana Obado akitoka mahakamani. Picha/ Richard Munguti

Waliposhtakiwa kiongozi wa mashtaka Bw Jacob Ondari na Alexander Muteti walimweleza , Jaji Lesiit kuwa , washukiwa hao wako na ushawishi mkubwa na wanapasa kuzuiliwa.

Ni Bw Obado tu aliyeachiliwa kwa dhamana ya Sh5milioni na kuamriwa awasilishe pasipoti yake mahakamani.

Mabw Oyamo na Obiero walinyimwa dhamana wakidaiwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani na Polisi umewalenga wao.

Jaji Lesiit alisema kuwa wawili hao wakiachiliwa kwa dhamana bila shaka watawavuruga mashahidi kwa lengo la kutweza haki na kulemaza ushahidi wa kesi hiyo.

“Ikiwa wataachiliwa kwa dhamana wawili hawa watafanya kila juhudi kuhakikisha haki imetoweka kwa kushawishi mashahidi wasifike mahakamani kutoa ushahidi,”alisema Jaji Lesiit.

Mabw Obiero na Oyamo walirudishwa gereza kuu la Kamiti hadi Januari 21 , 2019 hiyo itakaporudishwa.

You can share this post!

Akana kuondoa jina la katibu kwa kesi ya transfoma

Biashara yanoga Nakuru wafuasi wa Owuor wakijiandaa kwa...

adminleo