• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 10:55 AM
MOKAYA: Mourinho anafaa afurahie kutimuliwa

MOKAYA: Mourinho anafaa afurahie kutimuliwa

NA JOB MOKAYA

JUZI katika ukumbi huu, nilitabiri kwamba kufutwa kwa kocha wa zamani wa Manchester?United, Jose Mourinho lilikuwa suala la lini wala si iwapo.

Naam, ndiyo hayo yametimia. Mourinho alimwaga unga siku chache zilizopita.?Ingawa kuna picha za video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimwonesha Mourinho?akilia kama mtoto aliyepawa kichapo cha mbwa baada ya kuramba sukari, huenda kilio hicho cha Mourinho na machozi hayo yakawa machozi ya furaha.

‘The Special One’, kama anavyofahamika Mourinho, anajulikana kama kocha wa kuvuna mataji. Hali hiyo ilibadilika kabisa wakati huu kwani yeye hana tofauti na makocha wa timu?ndogo kama vile Fulham, Watford, Everton na hata Crystal Palace.

Kabla ya Mourinho kuondoka, hakukuwa na uwezekano wa Man-United kumaliza ndani ya timu nne bora msimu huu. Hata hivyo, huenda uwezekano huo ukarejea tena baada ya?Mourinho kupigwa kalamu na kocha mpya kudhihirisha uwezo wake kwa kushinda mechi mbili za kwanza.

Mourinho alipofutwa kutoka Chelsea misimu kadhaa iliyopita, huduma zake zilihitajika mahali?kwingi hata katika timu ya Arsenal. Mbali na kutakiwa Uingereza na kuishia Man-United, Mourinho alitakiwa na PSG ya Ufaransa, Real Madrid ya Uhispania, Inter Milan ya Italia, na klabu nyinginezo pamoja na timu za taifa.

Endapo Mourinho angeendelea kusalia Old Trafford na kisha kusajili matokeo mabaya kama yale, basi alikuwa na hatari ya kukataliwa na timu kubwa na kuishia kutoa huduma kwa timu za?chini kwenye jedwali au hata timu za daraja ya pili.

Kufutwa kwa Mourinho huko Chelsea kulimsaidia kupata milango mipya na kuishia kuingia ule wa Man-United. Kuendelea kukaa Man-United kungeendelea kudhihirisha namna?weledi wake ulivyofifia na namna makali yake yalivyopata kutu.?Jambo lililokuwa limesalia ili kuyaokoa maisha yake Old Trafford lilikuwa kupigwa kalamu sasa na kama si sasa, basi iwe sasa hivi.

Ubashiri huu tena ulitimia.?Apigwapo kalamu, ‘The Special One’ ambaye siye Special tena, ataonekana kwamba amedhulumiwa na klabu. Mashabiki wengi watamwonea imani na hata huenda akapata nafasi ya?kufunza timu nyingine yenye nafasi nzuri.?Je, umewahi kujiuliza ni nini kingalifanyika kama Mourinho angaliendelea kusalia Chelsea?wakati ule alipopigwa kalamu?

Lingekuwa janga kubwa ambalo halijawahi kutokea kwenye?historia ya soka. Historia yenyewe ingekuwa timu kushinda ligi msimu huu kisha kushushwa ngazi msimu?unaofuatia kwa kumaliza ya mwisho.

Naam, hivyo ndivyo ingalikuwa kwa Chelsea. Kabla ya Mourinho kufutwa, Chelsea ilikuwa katika nambari ya 15 ikiwa kwenye eneo la kushushwa?ngazi.

Na kama Mourinho angalisalia United, hali haingekuwa tofauti sana hapa. Ingawa haitakuwa haki kusema kwamba Manchester United ingeshushwa ngazi, ni haki kusema kwamba ingesajili matokeo duni sana labda kwenye hist oria ya timu hiyo.

Kufutwa kwa Mourinho hivyo basi kulikuwa afueni kwake kwani ataonewa imani na wengine watadhani kuwa kaonewa. Kuendelea kusalia kungekuwa na maana kwamba matokeo yakiwa duni basi hatapata timu nyingine ya haiba ya juu kusimamia.

You can share this post!

TAHARIRI: Serikali na KNUT wajali wanafunzi

Ilivyo, Liverpool hawana mshindani katika EPL na taji la...

adminleo