• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:55 AM
Sonko kutaja naibu huku waziri akidai kugeuzwa mke

Sonko kutaja naibu huku waziri akidai kugeuzwa mke

Na LEONARD ONYANGO

GAVANA wa Nairobi Mike Sonko Jumatano amesema kuwa atataja naibu wake kufikia Ijumaa huku waziri wa Elimu wa kaunti hiyo Bi Janet Ouko akilalamika kupewa majukumu ya mke na gavana huyo. 

Bw Sonko ambaye amekuwa akihudumu bila naibu kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, alisema ataunda upya baraza lake la mawaziri.

“Nitateua naibu wa wangu pamoja na kufanya uteuzi wa mawaziri kufikia Ijumaa,” akasema Bw Sonko aliyekuwa akihutubia wanahabari jijini Mombasa.

Wadhifa wa naibu wa gavana ulisalia wazi kufuatia kujiuzulu kwa Bw Polycarp Igathe aliyeondoka afisini Januari 2017 kutokana na alichosema kuwa kutoaminiwa naMnamo Agosti, Bw Sonko alisema kuwa ameorodhesha watu wanne, wote wanawake, ambao atateua naibu wa gavana miongoni mwao.

Miongoni mwa aliwaorodhesha ni Bi Agnes Kagure, Askofu Margaret Wanjiru, wakili Karen Nyamu na Bi Jane Weru.Alisema kuwa alikuwa bado anashauriana na rais na viongozi wa chama cha Jubilee kabla ya kutangaza rasmi na kuwasilisha jina la gavana mteule katika bunge la kaunti.

Mwaka 2018, Gavana Sonko alimteua wakili Miguna Miguna kuwa naibu wake lakini jina hilo likakataliwa na bunge la kaunti. Dkt Miguna anaishi uhamishoni nchini Canada.

2018, Bw Sonko alidai kuwa baadhi ya maafisa kutoka afisi ya rais wamekuwa wakimlazimisha kuteua watu fulani kuwa naibu wake.

Sonko amesalia na nusu ya mawaziri baada ya wengine kujiuzulu au kutimuliwa.Waziri wa hivi karibuni kujiuzulu ni Janet Muthoni Ouko aliyekuwa akisimamia wizara ya elimu.

Mawaziri watano waliosalia ni Bw Allan Igambi, Bw Charles Kerich, Bw Mohammed Dagane, Bw Newton Munene na Bw Larry Wambua.

Mawaziri walioteuliuwa mara tu baada ya Bw Sonko kuingia afisini 2018 ni Emmah Mukuhi (Mawasiliano), Peter Njuguna (Kilimo), Newton Munene (Biashara), Allan Igambi (Fedha), Hitan Majevdia (Afya),Vesca Kangogo (Ugatuzi), Janet Ouko (Elimu), Mohammed Dagane (Uchukuzi), Charles Kerich (Ardhi) na Larry Wambua (Mazingira). Mnamo Agosti Bw Sonko alimsimamisha kazi Majevdia kutokana na ‘uzembe’.

Mwezi mmoja baadaye Bw Sonko alimtimua Kangogo. Jumatano, Bw Sonko alidai kuwa Bi Ouko alifuja fedha za kufadhili masomo ya wanafunzi kutoka familia maskini kabla ya kujiuzulu Jumatatu.

Gavana alidai kuwa waziri wake huyo wa zamani alishirikiana na walaghai kuiba fedha hizo. Bi Ouko, hata hivyo, alikanusha madai hayo huku akisema kuwa Bw Sonko alimfanyisha kazi “kana kwamba amenioa’.

You can share this post!

Muafaka umeimarisha utalii nchini – Ripoti

TEKNOLOJIA: Mitandao ya kijamii inavyotumika kudunisha...

adminleo