• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Kidosho avunja kituo cha polisi akimtaka polisi kimapenzi

Kidosho avunja kituo cha polisi akimtaka polisi kimapenzi

MASHIRIKA na PETER MBURU

PENNSYLVANIA, AMERIKA

NGUVU za mapenzi huja na msisimko wa aina yake kwa watu wengi lakini kwa mwanamke mmoja kutoka Pennsylvania zilimsukuma kufanya yasiyotarajiwa.

Bi Ashley Keister wa miaka 27 alikuwa akimtaka kimapenzi afisa wa polisi, baada ya afisa huyo kumkamata mnamo Mei 2018. Bi Keister anasemekana kuwa alikuwa akimtumia jumbe kwenye mitandao ya kijamii afisa huyo, takriban mara 20 kila siku.

Mbali na hayo, alipohisi kuwa hayo hayatoshi, mwanamke huyo aliamua kuvunja katika kituo cha polisi alipohudumu afisa huyo na kuingia kwa nguvu ili apatane na mpenzio wake.

Kamera za CCTV zilimrekodi Bi Keister akivunja dirisha kwa kutumia kifaa cha kuhifadhi sigara ili kuingia katika kituo hicho usiku wa manane na kuanza kupitia faili wakati kituo hicho kilikuwa kimefungwa.

Hii ilikuwa licha yake kulazimishwa kutia saini mkataba kuwa hangemsumbua afisa huyo tena, awali siku hiyo ya Jumatatu.

Mkuu wa kituo hicho Curtis Nocera alisema kuwa mwanamke huyo alikuwa akichunguzwa kwa kumdhulumu kimapenzi afisa huyo.

“Alitaka kuwa na uhusiano naye. Nilimfanya kutia saini nakala iliyosema kuwa hangezungumza na afisa huyo ambaye amekuwa akimtumia jumbe Zaidi ya 20 kila siku,” akasema Bw Nocera.

Ilidaiwa kuwa Bi Keister alifanya hivyo akitarajia kuwa afisa huyo angejitokeza na kumkamata, kwani mbeleni alikuwa amepiga nambari 911, kabla ya kuvunja na kuingia kituoni.

Alipopigia polisi, aliwajulisha kuwa angeenda katika kituo husika, kisha akataka afisa huyo akutane naye kwa dakika kumi.

Baada ya kufanya hivyo, alisubiri polisi katika gari lake waje wamkamate, na alipomwona yule aliyemtaka alimkimbilia na kuanza kumrukia.

Jumatatu, alifikishwa kortini na kushtakiwa kwa kuvunja kituo kwa lengo la kijinai. Alifungwa katika jela ya Luzene ama faini ya dola 50,000.

You can share this post!

Korti yaamuru mkewe Linturi arudi kwa makazi ya Runda

Mtangazaji wa TV akaangwa kuvaa nguo yenye umbo la uume

adminleo