• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 6:55 PM
Mtoto wa miaka 13 ashangaza kuunda kampuni ya programu za kompyuta

Mtoto wa miaka 13 ashangaza kuunda kampuni ya programu za kompyuta

MASHIRIKA Na PETER MBURU

WELEDI wa mvulana mmoja wa miaka 13 kutoka taifa la India umeshangaza ulimwengu wa teknolojia baada yake kuanzisha kampuni ya programu za kompyuta.

Aadithyan Rajesh, mwanafunzi kutoka eneo la Kerala alianza upevu wa kiteknolojia akiwa mchanga na sasa weledi wake umezidi na kujulikana ulimwenguni baada ya hatua hiyo ya kihistoria.

Mtoto huyo alikuja na programu ya kwanza alipounda apu ya simu alipokuwa na miaka tisa kimchezo tu.

Mbali na kumiliki kampuni na kuunda apu, pia Rajesh hutengeneza logo na tovuti kwa wateja wake.

Mtoto huyo aliripotiwa na gazeti moja la Dubai kuwa alianza kutumia kompyuta alipokuwa na miaka mitano, jambo ambalo lilimpa maarifa mengi ya kutumia tarakilishi.

Kampuni aliyoanzisha inaitwa ‘Trinet Solutions’.

“Nilizaliwa Thiruvilla, Kerala kisha familia yangu ikahamia hapa nilipofikisha miaka mitano. Tovuti ya kwanza ambayo baba yangu alinionyesha ilikuwa BBC Typing, tovuti ya watoto kusoma na kuandika,” mtoto huyo akaeleza gazeti hilo la Dubai.

Hadi sasa, ameajiri watu watatu katika kampuni yake, wote ambao ni marafiki na wanafunzi wenzake.

“Nahitaji kufikisha miaka 18 ili kuwa mmiliki wa kampuni halisi. Hata hivyo, hata sasa tunafanya kazi kama kampuni tu. Tumefanya kazi na zaidi ya wateja 12 na kuwahudumia bila malipo,” akasema mtoto huyo.

You can share this post!

Teknolojia ya 5G kutetemesha mitandao 2019

Polisi lawamani kwa kumcharaza na kumjeruhi mwanamke

adminleo