• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
SHAMBULIO: Matukio makuu ya kigaidi awali hapa Kenya

SHAMBULIO: Matukio makuu ya kigaidi awali hapa Kenya

Na VALENTINE OBARA

MASHAMBULIO mengi ya kigaidi yametokea nchini Kenya tangu Jeshi la Taifa (KDF) lilipoingia Somalia kukabiliana na kundi la kigaidi la al-Shabaab chini ya Muungano wa Wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AMISOM) mnamo 2011.

Yafuatayo ni matukio makuu ya kigaidi ambayo yamewahi kutokea miaka ya juzi:

Agosti 7, 1998: Kundi la kigaidi la al-Qaeda lashambulia ubalozi wa Amerika katikati mwa jiji la Nairobi na kuua watu wapatao 213, wakiwemo raia kadhaa wa kigeni. Shambulio hilo kubwa la bomu lilisababisha maafa pia kwa watu waliokuwa ndani ya majengo yaliyokaribiana na ubalozi huo.

Novemba 28, 2002: Hoteli ya Kikambala yashambuliwa na watu 13 kuuawa. Ndege ya shirika la Arkia la Israeli yalirushiwa kombora ikiondoka katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Moi mjini Mombasa lakini ikakosa kuangushwa.

Septemba 21, 2013: Watu wasiopungua 67 wauawa kwenye shambulio lililotekelezwa na kundi la al-Shabaab katika jengo la kibiashara la Westgate, mtaani Westlands jijini Nairobi.

Juni 17, 2014: Watu wasiopungua 15 wauawa kwenye shambulio la kigaidi katika vijiji vya Majembeni na Poromoko, eneo la Mpeketoni, Kaunti ya Lamu.

Aprili 2015: Magaidi wa kundi la al-Shabaab wavamia Chuo Kikuu cha Garissa na kuua karibu watu 150.

You can share this post!

SHAMBULIO: Mitandao ya kijamii ilivyotumika kupasha...

Askofu aombwa akatae gari alilopewa na Ruto

adminleo