• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 10:55 AM
Sitaki kazi ya ukocha Man United – Southgate

Sitaki kazi ya ukocha Man United – Southgate

NA CECIL ODONGO

MKUFUNZI wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate amepuuzilia mbali habari zinazomhusisha na kutwaa kazi ya ukocha katika klabu ya Manchester United akisema lengo lake kuu ni kutambisha ‘The Three Lions’.

Manchester United waliagana na aliyekuwa kocha wao Jose Mourinho mwishoni mwa 2018 baada ya timu hiyo kuandikisha msururu wa matokeo mabaya na kumkabidhi mchezaji wao wa zamani Ole Gunnar Solskjaer kazi hiyo hadi mwisho wa msimu wa 2018/19.

Hata hivyo Gareth Southgate, Zinedine Zidane na Mauricio Pochettino ni miongoni mwa wakufunzi ambao wamekuwa wakihusishwa na kutwaa kazi ya kudumu ya ukufunzi kwenye klabu hiyo inayoshikilia nafasi ya sita katika msimamo wa jedwali la Ligi Kuu nchini Uingereza(EPL).

Akishiriki mahojiano na Sky Sports, Southgate alisema kwamba haoni akirejelea ukufunzi katika kiwango cha klabu hivi karibuni kwa kuwa anazingatia kazi yake akilenga kufanya makuu na kuipeleka Uingereza mbali.

“Mimi ndiye meneja wa Uingereza nafasi ambayo ni kama tunu na hidaya kwangu. Tumekuwa na mwaka bora zaidi baada ya kipindi cha miaka 28. Tupo na mechi za nusu fainali ya ligi ya Mataifa ya bara uropa(Nations League) mwaka huu na taifa bingwa barani Uropa mwaka ujao wa 2020 ugani Wembly iwapo tutafuzu,” akasema Southgate.

You can share this post!

David Luiz na wenzake wasimama na Sarri licha ya vichapo

Ngono ni muhimu sana katika maisha ya uzeeni, aeleza ajuza

adminleo