• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 12:30 PM
Menengai Cream Homeboyz inavyokuza vipaji vya raga

Menengai Cream Homeboyz inavyokuza vipaji vya raga

NA RICHARD MAOSI

KIKOSI cha Menengai Cream Homeboyz almaarufu kama Deejays kilibuniwa 2009 ili kuwaendeleza vijana wenye motisha katika mchezo wa raga.

Waanzilishi walitarajia kuzalisha zana mashuhuri kutoka humu nchini bila kutegemea huduma za kigeni.

Wao hufanya mazoezi katika uwanja wa Jamhuri Showground mjini Nairobi kila siku za wiki wakishirikisha timu ya kwanza na ile ya chipukizi wasiozidi miaka 20.

Kufikia sasa idadi ya wachezaji imetimu 46, ushindani mkali ukishuhudiwa timuni huku kila mmoja akiwania kwa pupa kupata nafasi katika kikosi cha kwanza.

Mnamo 2015 Homeboyz walipata ufadhili kutoka kampuni ya Menengai oil Refineries na ndipo wakapata jina la Menengai Cream Homeboyz.

Kuanzia hapo wachezaji wa Homeboyz wamepata mafanikio mengi na kujijengea jina ndani na nje ya taifa.

Kulingana na mkufunzi Simon Odongo anasema hakuna kitu kizuri kama kushughulikia maslahi ya wachezaji.

“Kutambua na kulea vipaji ni jambo jingine lakini zaidi ya yote tunawahimiza wachezaji wenye talanta wasikate tamaa, licha ya changamoto za hapa na pale juhudi zao zitawafikisha mbali,”alisema.

Miundo msingi bidii, maslahi na ushirikin baina ya wachezaji unazidi kunogesha ladha ya raga humu nchini.Hasa tukiangazia mafanikio ya kikosi cha Homeboyz.

2013 Homeboyz walinyakua taji la Kabeberi 7s. Hawakukomea hapo waliendeleza mizungu kishaye wakashinda Kisii 7s 2014.

Mataji mengine ni Masaku ambapo walifikia katika awamu ya semi fainali katika mashindano yaliyobatizwa jina la Impala Floodlit.

Mpangilio mzuri wa miundo mbinu pamoja na ushirikiano baina ya wachezaji na kocha ndio siri ya ufanisi wao. Matokeo mazuri yamewafanya kuwatoa wachezaji wanaowakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa kwa timu ya Simba.

Mwaka uliopita wachezaji 12 walitajwa katika kikosi kilichowakilisha Kenya katika Dubai 7s. Bush Mwale, Mark Wandeto na Cyprian Kuto waliongoza timu.

“Uzuri wa kushiriki ligi za kimataifa kunasaidia kuwanoa wachezaji na kuwapatia uzoefu wa aina yake,ingawa wanaweza kupoteza mchuano mingine huwa wamejiongezea tajriba,”Odongo alisema.

Kwa mujibu wa nahodha wa kikosi Thomas Okidia,wanaendelea kujipiga msasa ili kuhakikisha wanayahifadhi mataji yao na kushinda matuzo zaidi.

Anaungama watani wao jadi ni timu kama vile Black Blad,KCB,Oilers, Mwamba na Nondies.

Kenya Rugby Union ilitoaoa ratiba ya michuano kote nchini mnamo 2018-2019 na Homeboyz ilishirikishwa katika michuano hiyo,

Kwa sababu hiyo Homeboyz walinyakua taji lao la kwanza wachezaji 15 kila pande mnamo 2018 wakibeba taji la Kenya Cup walipobamiza Impala 21-3, katika uwanja wa RFUEA.

.Baadae tarehe 29 Novemba 2018 Homeboyz walijizatiti na kupata nafasi ya kushiriki katika ngarambe za Samurai fixtures nchini Afrika kusini.

Upekuzi wetu ulibaini mchezo wa raga kwa wachezaji 7 kila upande ndio wanaopokea malipo mazuri kuliko mchezo mwingine nchini.

Michuano ya raga huwa na msimu mmoja kinyume na kandanda inayoshiriki misimu miwili ya nyumbani na ugenini.

Aidha endapo Kenya itafanya vizuri katika michuano ya hadhi kubwa katika tasnia ya kimataifa na kumaliza nambari 15 basi kila mchezaji anaweza kutia kibindoni hadi zaidi ya laki mbili.

Menengai Cream Homeboyz ni klabu inayokuwa kwa kasi kubwa nchini Kenya. Ndio maana imekuwa na uwezo wa kuwaleta pamoja wachezaji wa haiba kubwa kote duniani.

Homeboyz huwapatia kazi katika viwanda baadhi ya wachezaji wake mbali na kuwalipia karo wanaosomea taaluma mbalimbali chuoni.Mchezo wa raga una kanuni zake cha msingi ni ukufunzi kucheza na kupata mataji.

Bila kufuata kanuni hizi mchezaji hana nafasi ya kutamba katika ulingo wa mchezo wa raga.

Wachezaji wengi wa Homeboyz bila shaka wanaelezea haja yao kubwa kucheza raga katika rubaa za kimataifa wakiamini watajiendeleza.

Nchi kama vile New Zealand, Uingereza na Canada zimepatia michezo nafasi kubwa na hata kushirikisha michezo kama somo la kutahiniwa hadi mtu akahitimu ukufunzi.

Hivi sasa wakijiandaa kwa ajili ya kivumbi kikali kuanzia Februari 17 hadi Mei 2019. Ligi hiyo ya Kenya itakayoshirikisha makundi mawili ya timu sita katika kila kundi.

Homeboyz wakiwa katika kundi E kukabana koo na KCB katika mechi ya ufunguzi.

Wameelezea matumaini kuhifadhi taji lao ifikiapo mwisho wa michuano hiyo.

You can share this post!

SACHANGWAN: Kaburi la umma lilivyogeuka kitega uchumi kwa...

SACHANGWAN: Barabara ya mauti yaboreshwa

adminleo