• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 3:25 PM
China yazindua apu inayotambua mtu wa madeni akiwa karibu

China yazindua apu inayotambua mtu wa madeni akiwa karibu

MASHIRIKA Na PETER MBURU

SERIKALI ya China imetengeneza apu ambayo ina uwezo wa kufahamisha mtu ikiwa alipo kuna mtu mwenye madeni.

Gazeti la serikali, China Daily, majuzi lilitangaza kuwa maafisa wa mkoa wa Hebei waliunda apu hiyo kwa jina ‘map of deadbeat debtors’, ambayo inapatikana kupitia mtandao wa kijamii wa WeChat, unaotumika katika taifa hilo.

Inavyofanya kazi apu hiyo ni kuwa inaanza kuwaka wakati iko umbali wa mita 500 karibu na mtu aliye na madeni, gazeti hilo lilidai.

Vilevile, inaashiria mahali halisi ambapo anayedaiwa yuko, japo haikuwa wazi ikiwa inaeleza habari za kibinafsi kumhusu mdaiwa kama jina, picha na vitambulisho vingine.

Ikidaiwa kuwa inayolenga kuwafanya watu kuwa macho na watu wenye madeni, bado haijafafanuliwa hata hivyo ukubwa wa deni ambao mtu anafaa kuwa katika ili kumulikwa na apu hiyo.

Gazeti la China Daily lilisema apu hiyo itawafanya watu kuwaanika watu wenye madeni, ambao wana uwezo wa kuyalipa.

Katika utamaduni wa China, kuweka hazina hutiliwa maanani kuliko kutumia pesa, huku kukopa madeni kukiwa mwiko.

Mfumo mpya wa China ambao utaanza kazi mwaka ujao utakua ukikagua mtu kuhusu kiwango chake cha uaminifu na tabia anapokuwa katika mbinu za usafiri wa umma ili kumpa deni.

You can share this post!

Gavana azindua barabara ya lami kuwafaa wakulima

MENENGAI CRATER: Mali asili inayofumbiwa macho na serikali

adminleo