• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 9:15 PM
Mwalimu aliyenajisi mtoto hadi akamharibu utumbo asubiri kunyongwa

Mwalimu aliyenajisi mtoto hadi akamharibu utumbo asubiri kunyongwa

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MWALIMU kutoka kuzimu ambaye alimnajisi mwanafunzi kwa fujo hadi akamharibu utumbo na kufanyiwa upasuaji kutibiwa nchini India atanyongwa hapo Machi, mahakama imeamua.

Bw Mahendra Singh Gond atakuwa mtu wa kwanza kuuawa tangu sheria ilipobadilishwa mwaka 2019 na kuweka hukumu ya kifo kwa watu wanaonajisi watoto.

Mfungwa huyo alisemekana kumvamia mtoto huyo mnamo Juni mwaka uliopita na kumteka nyara, kisha akampeleka hadi msituni ambapo alimnajisi na kumtesa, kisha akamuacha huko akidhani amekufa.

Mahakama Kuu ya India ilithibitisha hukumu hiyo ya kifo mwezi uliopita, ikiamua kuwa mwalimu huyo atanyongwa mnamo Machi 2.

Mtoto huyo alidaiwa kulala miezi kadha katika hospitali ya New Delhi ambapo alikuwa akifanyiwa upasuaji, kwani utumbo wake ulikuwa umeharibiwa vibaya.

Kwa sasa, Gond yuko katika jela ya Jabalpur, kati mwa India.

Wakidhibitisha hukumu hiyo, majaji walisema “Korti haziwezi kuepuka jukumu lao la kuadhibu wakora wabaya ili kuzuia visa vingine vya jinai kama hiki.”

“Mtu anayehusika ni mwalimu ambaye anafaa kufunza maadili kwa wanafunzi na hivyo kisa hiki kina umuhimu,” wakasema.

Mwaka uliopita, sheria ya nchi hiyo ilibadilishwa ili kila mtu anayepatikana na hatia ya kunajisi watoto wa chini ya miaka 12 wawe wa kunyongwa.

Visa vya dhuluma za kingono nchi hiyo vimekidhiri tangu 2012, jambo ambalo lilipelekea sheria kubadilishwa.

You can share this post!

Aua bosi wake kupinga masharti makali ya kazi

Aapa kuwashtaki wazazi wake kwa kumzaa bila idhini

adminleo