• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:33 AM
Wakenya sasa wanatumia umeme zaidi

Wakenya sasa wanatumia umeme zaidi

Na BERNARDINE MUTANU

Matumizi ya umeme nchini yameendelea kuongezeka kutokana na ripoti mpya. Katika muda wa miaka minne, matumizi ya umeme Novemba nchini yalikuwa masaa 750.97 Gigawatt (GWh).

Matumizi hayo ni ishara tosha kuhusiana na ukuaji wa uchumi nchini. Kulingana na data kutoka Shirika la Takwimu nchini (KNBS), kiwango hicho kilikuwa cha juu zaidi kutoka 2015 ambapo katika mwezi wa Mei, kiwango cha umeme uliotumiwa kilikuwa ni 826.76 GWh.

Kulingana na kaimu meneja msimamizi wa Kenya Power Bw jared Othieno, kiwango hicho cha matumizi ya juu kilitokana hasa na viwanda ambavyo vilihitaji kutengeneza bidhaa zaidi kwa sababu ya sikukuu.

“Novemba kwa kawaida huwa ni mwezi ambapo huwa na mahitaji mengi ya bidhaa kwa sababu ya sikukuu. Mahitaji hayo hupungua Desemba viwanda vinapofungwa ili watu kwenda sikukuu,” alisema.

Pia, kulikuwa na matumizi mengi ya umeme Januari, alisema Bw Othieno. Wenye viwanda ambao hutengeneza bidhaa wakati wa usiku wameendelea kunufaika baada ya serikali kuwapunguzia ada ya umeme.

You can share this post!

Mgomo wa JKIA ulivyozimwa

Ebrahims yatia kikomo kwa biashara ya miaka 75

adminleo