• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 4:36 PM
Kenya yashuka viwango vya FIFA hadi 106

Kenya yashuka viwango vya FIFA hadi 106

Na GEOFFREY ANENE

KENYA imeteremka nafasi moja katika viwango bora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) vilivyotangazwa Alhamisi.

Katika viwango hivi vya mataifa 204, Harambee Stars ya kocha Sebastien Migne sasa inashikilia nafasi ya 106.

Kuteremkwa kwake kumechangiwa na matokeo ya Kombe la Bara Asia ambayo yamefanya Jordan kuruka juu nafasi 12 kutoka 109 hadi nambari 97 baada ya kufika raundi ya 16-bora nchini Milki za Kiarabu hapo Januari 20, 2019.

Viwango hivi ndivyo vya kwanza mwaka 2019. Vilikuwa vimetangazwa mara ya mwisho Desemba 19, 2018.

Hakuna mabadiliko katika nafasi 20 za kwanza duniani, huku Ubelgiji, mabingwa wa dunia Ufaransa pamoja na Brazil, Croatia, Uingereza, Ureno, Uruguay, Uswizi, Uhispania na Denmark zikifuatana katika nafasi kumi za kwanza.

Timu 16 za kwanza barani Afrika zimeathirika pakubwa na matokeo ya Bara Asia. Zimeshuka kati ya nafasi moja na mbili, huku Senegal ikisalia nambari moja na kufuatiwa na Tunisia, Morocco, Nigeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) katika usanjari huo barani Afrika.

Uganda ni nambari moja katika eneo la Afrika Mashariki na Kati almaarufu Cecafa. Imeteremka nafasi mbili hadi nambari 77 duniani.

Kenya, ambayo itamenyana na Ghana katika mechi yake ya mwisho ya kufuzu kushiriki Kombe la Bara Afrika (AFCON) mwezi ujao, inasalia ya pili Cecafa katika nafasi ya 106 duniani baada ya kushuka chini nafasi moja.

Viwango bora vya Bara Afrika (mataifa 23-bora):

1.Senegal (chini nafasi moja hadi 24 duniani)

2.Tunisia (chini nafasi mbili hadi 28 duniani)

3.Morocco (chini nafasi tatu hadi 43 duniani)

4.Nigeria (chini nafasi mbili hadi 46 duniani)

5.DR Congo (chini nafasi mbili hadi 51 duniani)

6.Ghana (chini nafasi moja hadi 52 duniani)

7.Cameroon (chini nafasi moja hadi 56 duniani)

8.Misri (chini nafasi moja hadi 57 duniani)

9.Burkina Faso (chini nafasi moja hadi 62 duniani)

10.Mali (chini nafasi moja hadi 65 duniani)

11.Ivory Coast (chini nafasi moja hadi 66 duniani)

12,Guinea (chini nafasi mbili hadi 68 duniani)

13.Algeria (chini nafasi mbili hadi 69 duniani)

14.Afrika Kusini (chini nafasi mbili hadi 74 duniani)

15.Cape Verde (chini nafasi mbili hadi 74 duniani)

16.Uganda (chini nafasi mbili hadi 77 duniani)

17.Zambia (juu nafasi moja hadi 82 duniani)

18.Congo Brazzaville (imetulia 84 duniani)

19.Gabon (imekwamilia 85 duniani)

20.Benin (haijasonga kutoka 94 duniani)

21.Mauritania (imesalia 101 duniani)

22.Libya (imeshuka nafasi moja hadi 105 duniani)

23.Kenya (imeteremka nafasi moja hadi 106 duniani)

34.Sudan (imesalia 127 duniani)

36.Rwanda (imepaa nafasi mbili hadi 135 duniani)

37.Tanzania (imeruka juu nafasi moja hadi 137 duniani)

38.Burundi (imeimarika kutoka 139 hadi 138 duniani)

45.Ethiopia (imekwamilia 151 duniani)

47.Sudan Kusini (haijasonga kutoka 164 duniani)

52.Djibouti (imekwamilia 197 duniani)

53.Somalia (imesalia 204 duniani)

53.Eritrea (imekwamilia 204 duniani)

You can share this post!

Wanaume ‘singo’ hutoa uvundo unaowavutia...

Sharks kutetea ubingwa wa SportPesa Shield

adminleo