• Nairobi
  • Last Updated April 23rd, 2024 9:40 PM
Ushindi wapandisha Wazito hadi kileleni NSL

Ushindi wapandisha Wazito hadi kileleni NSL

Na JOHN ASHIHUNDU

Ushindi wa Wazito FC wa 2-1 dhidi ya Fortune Sacco mwishoni mwa wiki uwanjani Camp Toyoyo, Nairobi umewasukuma hadi kileleni mwa Ligi ya Taifa (NSL).

Matokeo hayo kadhalika yamepandisha idadi ya pointi zao kufika 31 kutokana na mechi 13, moja mbele ya Ushuru ambao walitoka sare 1-1 na Kisumu All Stars katika mechi nyingine iliyochezewa Ruaraka.

Kwingineko, Shabana iliandisha ushindi wa kwanza baada yak wend mechi saba bila ushindi. Vijana hao kutoka Nyanza waliitandika Kenya Police 4-1 katika mechi iliyochezewa Camp Toyoyo.

Chini ya kocha mshikilizi, Andrew Kanuli, Shabana imepanda imepanda kutoka nafasi ya 10 hadi ya saba judwalini, sawa na Kenya Police walio na upungufu wa mabao.

Kanuli alieleza furaha yake kufuatia ushindi huo mkubwa huku akiwataka wachezaji wake waendelee kuandikisha matokeo mema katika mechi zilizobakia.

“Nawapongeza wachezaji kwa bidi yao wakati huu tukijipanga kwa mechi ya kesho mjini Thika dhidi ya wenyeji Fortune Sacco,” Kanuli alisema.

Nairobi Stima waliendelea kubakia katika nafasi ya tatu licha ya kutoka sare 1-1 na Nairobi City Stars mjini Naivasha.

Stima chini ya kocha George Owoko ndio timu pekee ligini humo ambayo haijashindwa, huku FC Talanta walioagana bila kufungana na St Joseph’s Youth wakiimiliki nafasi ya nne.

Kangemi All Stars ambao walichapwa 3-1 na Administration Police wanakamatai nafasi ya mwisho wakiwa na pointi nne.

Migori Youth walio katika nafasi ya 18 walinyukwa 2-1 na Thika United na kuendelea kubakia katika nafasi mbaya sawa na Green Commandos na Kangemi All Stars.

Matokeo ya mechi za NSL kwa ufupi yalikuwa:

Bidco United 1 Coast Stima 0; Green Cammandos 0 Kibera Black Stars 1; Eldoret Youth 0, Modern Coast Rangers 1; Ushuru 1 Kisumu All Stars 1; Administaration Police 3 Kangemi All Stars 1; Thika United 2 Migori Youth 1; FC Talanta 0 St Joseph’s Youth 0; Nairobi Stima 1 Nairobi City Stars 1; Shabana 4 Kenya Police 1.

You can share this post!

Sababu ya serikali kukataa kusajili gari la Dave Assman

Valentino kuadhimishwa kwa utoaji wa damu

adminleo