• Nairobi
  • Last Updated April 19th, 2024 3:03 PM
EACC yamsifu Waititu kwa utendakazi wa kaunti yake

EACC yamsifu Waititu kwa utendakazi wa kaunti yake

Na LAWRENCE ONGARO

TUME ya Kupambana na Ufisadi nchini (EACC) imeipongeza Kaunti ya Kiambu kwa utendakazi wake.

Katibu wa tume hiyo Bw Twalib Mbarak alisema hata ingawa kuna matatizo ya hapa na pale Kaunti ya Kiambukwa uongozi wa Gavana Ferdinand Waititu imetekeleza wajibu wake inavyostahili.

Alisema kwa muda wa miezi kadha wamekuwa wakiendesha uchunguzi wao kuhusu utendakazi wa Kaunti hiyo kupitia matumizi ya pesa.

Kuhusu maswala ya kukusanya pesa za ushuru, walidai fedha nyingi hazirejeshwi kwenye hazina ya kaunti hiyo kwa ukosefu wa uwajibikaji.

Kaunti hiyo imeshauriwa kutumia vifaa vya teknolojia aina ya dijitali ili kupata ushuru ipasavyo.

Maswala ya kutoa zabuni kwa umma ilidaiwa inatashwishi lakini yaweza kurekebishwa kwa kufuata uwajibikaji.

Kaunti ilishauriwa kuweka mikakati maalum ili kuepukana na kupotea kwa pesa kiholela wakati wa malipo ya mishahara ya wafanyi kazi.

Spika wa bunge la Kaunti hiyo Bw Stephen Ndichu alisema wataweka mikakati kuhakikisha hakuna diwani yeyote atakayelipwa fedha za bure bila kuzitolea jasho.

“Diwani yeyote atakayekosa kufika kazini kirasmi ama akikosa kusafiri na wenzake kwenye ziara maalum hatakubaliwa kupokea marupurupu yoyote . Ninayasema haya mbele ya tume ya EACC,” alisema Bw Ndichu.

Gavana wa Kiambu Bw Ferdinand Waititu alisema tayari waliondoa majina ya wafanyi kazi gushi 240 waliokuwa katika orodha ya wakanyi kazi wa kawaida.

Aliiomba tume hiyo imsaidie kupambana na wanyakuzi wa ardhi.

Alisema tayari amefanya juhudi kuona ya kwamba iliyokuwa kampuni ya Uplands Bacon Factory inaregeshwa kwa kaunti ya Kiambu.

Wakati huo pia alifanya juhudi kuona ya kwamba eneo la kuchimba madini ya Diatomites la Ndeiya linaregeshwa kwa kaunti ya Kiambu.

“Serikali ya kaunti ya Kiambu itaendelea kufanya kazi nanyi EACC na wakati wowote tukiwa na jambo tutafanya juhudi kuwajulisha ili tupate mwongozo kamili,” alisema Bw Waititu.

 

You can share this post!

2022: Ruto hapumui, pingamizi dhidi yake zapamba moto

Magunia 222 ya bangi yanaswa Kiambu

adminleo