• Nairobi
  • Last Updated April 16th, 2024 1:25 PM
Lugari Blue Saints yasaka ubingwa wa Chapa Dimba na Safaricom

Lugari Blue Saints yasaka ubingwa wa Chapa Dimba na Safaricom

Na JOHN KIMWERE

BAADA ya timu ya wavulana ya Lugari Blue Saints kuibuka mabingwa wa Chapa Dimba na Safaricom Season Two Mkoani Magharibi, sasa inapania kushusha kimbunga kikali katika fainali za kitaifa zitakaoandaliwa katika Kaunti ya Meru hapo Juni mwaka huu, na kuibuka mibabe wa kitaifa.

Kikosi hicho chini ya kocha, Ted Amnala kilijipatia tiketi hiyo baada ya kuibuka wafalme wa Mkoa wa Magharibi kilipotandika The Saints kwa mabao 2-1 katika fainali iliyopigiwa uwanjani Bukhungu Stadium, Kakamega.

Kwenye nusu fainali Lugari Blue Saints ilinyorosha Bukembe Boys kwa mabao 2-0 nayo The Saints ilinasa ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Ebbu Stars.

Kwa sasa wavulana hao wamezamia mazoezi makali kujiweka vizuri kukabili wapinzani wao katika fainali za kitaifa.

Kocha wa Lugari Blue Saints akibebwa juu na wanafunzi wa shule wakisherekea ushindi wa wenzao kwenye taji la Chapa Dimba na Safaricom, Season Two. Picha/ John Kimwere

Kocha huyo amepongeza wavulana hao kwa kazi jema waliofanya kwenye michezo ya msimu huu.

“Bila shaka nashukuru wachezaji wangu wote kwa kuonyesha mchezo mzuri pia kushirikiana dimbani maana kama haingekuwa kujitolea kwao hawangefikia hadhi hiyo,” alisema na kuongeza kwa sasa analenga kuona wachezaji wake kadhaa wakiteuliwa katika kikosi cha kitaifa kitakachokwenda nchini Uhispania kushiriki mechi za kupimana nguvu na klabu tofauti katika taifa hilo.

Kadhalika alisema ufanisi wao ulichangiwa pakubwa na jinsi walivyojitolea kushiriki mazoezi nyakati za asubuhi na jioni. La mno alidokeza kwamba nyakati zote walikuwa wakianza na maombi kwa Mwenyezi Mungu ili kuwasaidia kutimiza ndoto yao.

Cyprian Mangeni (kushoto) wa The Saints ikimchenga Gideon Nakaya wa Ebbu Stars kwenye mechi ya wavulana ya nusu fainali ya Safaricom Chapa Dimba Season Two, Western Region Uwanjani Bukhungu Stadium, Kakamega. The Saints ilishinda magoli 4-0. Picha/ John Kimwere

Lugari Blue Saints inajivunia kushinda zaidi ya mechi 15 kwenye kampeni hizo. Wavulana hao hawakupoteza mchezo wowote pia katika mechi zote walizoshiriki walifungwa zaidi ya mabao 27 na kufungwa bao moja pekee.

Hata hivyo, alisema anashangaa sana maana licha ya wavulana hao kutwaa taji hilo la Mkoa huo hawajamuona Mbunge wa eneo hilo, Ayub Savula angalau akifika kuwashukuru kwa kufanya vizuri.

Kocha huyo anashukuru wazazi na jamii ya eneo hilo kwa jumla kwa kuwaunga mkono kuanzia mwanzo hadi mwisho walipotawazwa washindi.

Brian Lusamukha (kulia) wa Lungari Blue Saints akisherekea baada ya kufungia timu hiyo bao la kwanza walipokutana na Bukembe Friends kwenye nusu fainali ya wavulana kuwania taji la Safaricom Chapa Dimba Season Two, Western Region Uwanjani Bukhungu Stadium, Kakamega. Lungari Blue Saints ilishinda mabao 2-0. Picha/ John Kimwere

Kocha huyo anasema anafahamu fainali zitakuwa gumu haitakuwa mteremko huku akidai wanatarajia upinzani mkali kutoka timu itakayoibuka mshindi katika Mkoa wa Nyanza.

Hata hivyo anasema ingawa hawawezi kupuuza timu yoyote itakayofuzu kwa fainali za mwaka huu lakini ana imani tosha wachezaji wake wanaouweza kufanya kweli na kutwaa ubingwa wa kitaifa. Mabingwa wa kitaifa katika ngarambe hiyo watatuzwa kitita cha Sh1 milioni kando na zawadi zingine.

Wavulana hao walituzwa Sh200,000 kwa kuibuka mabingwa wa taji hilo eneo hilo pia kusahau kitengo cha wasichana ambapo ushindi uliwaendea wachezaji wa Bishop Njenga Girls.

You can share this post!

EMMAH NJERI: Anawataka wasanii wakomeshe umbea na kupakana...

LEUSHADORN LUBANGA: Afichua kutamaushwa na waigizaji wa...

adminleo