• Nairobi
  • Last Updated April 20th, 2024 6:55 AM
Ushuru FC yapaa NSL

Ushuru FC yapaa NSL

NA CECIL ODONGO

USHURU FC Jumamosi Februari 23 ilipaa hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la Ligi ya Supa (NSL) baada ya kushinda Nairobi City Stars 2-0 katika uwanja wa Camp Toyoyo.

Ushindi huo uliwawezesha vijana wa kocha Ken Kenyatta kusitisha rekodi mbovu ya kutopata alama tatu katika mechi zao tatu zilizopita na kupunguza mwanya kati yao na viongozi Wazito FC hadi alama alama tatu.

Wazito walikosa kutumia vyema uwanja wao wa Camp Toyoyo pale walipokabwa sare ya 1-1 na Administration Police.

Shabana FC ambao kocha wao Gilbert Selebwa alipata nafuu kwa kuondolewa marufuku ya mechi na faini na Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la soka nchini(FKF), nao walipata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Thika United na kupaa hadi nafasi ya sita ligini.

Nairobi Stima hata hivyo waliendelea kushikilia kukutu nafasi ya tatu baada ya kuwalaza Kibera Black Stars 2-0 ugani Camp Toyoyo kabla ya kupisha mechi ya Kangemi All Stars dhidi ya St Joseph Youth uwanjani humo, mchuano ambao uliishia sare ya 1-1.

Green Commandoes ya Kakamega ilitoka mkiani mwa NSL hadi nafasi ya 18 kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Eldoret Youth katika uwanja wa Bukhungu.

Katika  mechi nyingine,  Modern Coast Rangers ilishinda  Coast Stima 1-0,  Bidco United ikasajili matokeo kama hayo ikipambana na Fortune Sacco, Kenya Police ikachapa Kisumu All stars 2-1 nao Migori Youth wakakamilisha raundi ya 14 ya NSL wikendi kwa sare ya 1-1 dhidi ya FC Talanta mjini Awendo.

You can share this post!

‘Team Tangatanga’ yafufuka

Raha kwa Lions Eye Hospital FC kupata pointi tatu

adminleo