• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 11:42 PM
Demu mfyonzaji atemwa na sponsa

Demu mfyonzaji atemwa na sponsa

Na John Musyoki

KIANGINI, MAKUENI

KIPUSA mmoja kutoka eneo hili alifurushwa na sponsa wake mkahawani kwa kuwa na mahitaji chungu nzima.?

Duru zinasema demu alikuwa ameishi na sponsa huyo kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuhitimu masomo yake katika chuo kikuu.

Siku ya kioja, wawili hao walikuwa wakijumuika pamoja mkahawani, demu aliposikika akiitisha vitu vingi vya bei ghali.

“Beib, najua unanipenda na una uwezo wa kunifanyia kila kitu. Nina ombi moja kwako. Ningependa unijengee nyumba ya kifahari, uninunulie gari langu na unifungulie biashara mjini. Kumbuka nimehitimu na shahada na nina uwezo wa kuendesha biashara vizuri,” demu alimwambia sponsa.

Inasemekana buda alijishika tama huku akiwaza na kuwazua baada ya demu kumwarifu yaliyokuwa moyoni.

“Kwa nini unajishika tama. Ulipokuwa unanitongoza uliniambia utanifanyia kila kitu. Umeduwaa kwa sababu gani, zungumza,” demu alimwambia sponsa.

Baadaye buda aligutuka mawazoni na kumkemea demu. “Wewe, unasema nini sasa. Kwanza sijakuoa rasmi na unadai nikufanyie mambo hayo yote. Sina pesa na uliyodai hayawezekani kamwe kwa wakati huu. Tuvumiliane na upambane na hali yako,” jamaa alimwambia demu.

“Eti nipambane na hali yangu. Kwa hivyo umefilisika!” demu alifoka kwa mshangao.

Kwa upande wa buda alipandwa na hasira kupita kiasi na akaamua kumtema mrembo papo hapo.

“Kuanzia sasa sitaki kukuona karibu na mimi. Kwenda kabisa na usiwahi kuja kwangu kwa sababu sasa umeanza kuharibu mambo,”buda alifoka.

Demu kuona jinsi jamaa alivyoonyesha hasira nyingi alitoka shoti na kupotelea vichochoroni. Hata hivyo haikujulikana kilichojiri baada ya kioja hicho.

You can share this post!

Shinikizo Rotich ang’atuke zazidi

MUTANU: Serikali isilegeze kamba katika uhifadhi wa misitu

adminleo