• Nairobi
  • Last Updated April 25th, 2024 7:25 PM
UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Maendeleo ya Kiswahili katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Maendeleo ya Kiswahili katika nyanja ya Sayansi na Teknolojia

Na MARY WANGARI

TAFITI nyingi za wasomi anuwai mathalani Qorro (2005), Malekela (2003 & 2004), na Mwinsheikhe (2003), zinajadili kuwa, matumizi ya lugha ya kigeni katika kufundishia yana madhara makubwa kwa ujenzi wa jamii imara.

Hii hudhihirika katika maendeleo katika nyanja anuwai za kiuchumi, kijamii, kisiasa na ukuzi wa sayansi na teknolojia.

Yote haya ni kwa sababu wanafunzi hukosa kupata stadi kamili za somo husika.

Aidha, Mwinsheikhe (2003), anadai kwamba, hali ya walimu wengi kutotumia lugha ya Kiswahili kufundishia masomo yote huchangia kutokueleweka vyema kwa kile wanachofundisha darasani.

Hii hasa hutokana na kwamba hawana umilisi wa kutosha wa lugha ya Kiingereza.

Hivyo hulazimika kufikiri na kuunda dhana zote kwa Kiswahili kisha kuzitafsiri kimawazo katika akili zao katika Kiingereza ambacho dhana zake kuhusu mambo wanayojifunza hazimo akilini mwao tangu awali.

Matokeo yake ni kwamba, dhana zinazoundwa akilini siyo sahihi kutokana na mawasiliano kiakili kukwazwa na lugha wasio na ujuzi wake.

Nchini Tanzania kwa mfano, masomo na mafunzo hufunzwa kwa Kiingreza na Kiswahili kinyume cha matakwa ya sera.

Wanafunzi wengi wanapojifunza wao wenyewe nje ya darasa hutumia lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa kiasi fulani.

Hii inaonyesha kuwa, Kiswahili ndiyo lugha inayoeleweka kwa wanafunzi na walimu.

Vilevile, Mekacha (2000), anasema kwamba, watoto wengi, hata wa vijijini wanakuwa wanafahamu vizuri lugha ya Kiswahili wanapoanza masomo ya shule ya msingi.

Kompyuta

Msanjila na wenzie (2009), wanasema kuwa, hadi wakati huu, lugha ya Kiswahili imekwisha ingizwa katika mifumo miwili ya kompyuta inayojulikana kama Linux na Microsoft.

Msanjila na wenzie wanadai kwamba, kuingizwa kwa Kiswahili katika mifumo hii maana yake ni kwamba mtumiaji anaweza kuvinjari mifumo hiyo ya kompyuta kwa Kiswahili akiamua kufanya hivyo, na isitoshe ni kielelezo cha ukuaji wa lugha hiyo.

Aidha, wanasema kuwa uwezo wa Kiswahili kuingia katika teknolojia ya habari na mawasiliano, kunawathibitishia wenye mamlaka na jamii kwa ujumla kwamba Kiswahili kina uwezo wa kukabili hata mambo yasiyokuwa ya asili yake.

Baruapepe ya Mwandishi: [email protected]

Marejeo

Rugemalira, J. M. (2005). Theoretical and Practical Challenges in a Tanzanian English Medium School. Africa and Asia.

Senkoro, F. (2004). The role of language in education and poverty alleviation: Tool for access and empowerment in Justian Galabawa and Anders Narman Education poverty and Inequality (Eds.). Dar es Salaam: KAD Associates.

Skutnabb-Kangas, T. & McCarty, T. L. (2008). Key concepts in bilingual education: Ideological, historical, epistemological and empirical foundations. In J. Cummins and N. H. Hornberger (Eds.), Encyclopedia of Language and Education, 2nd Edition, Volume 5: Bilingual Education. New York: Springer Science + Business Media LLC.

You can share this post!

Wakazi 2,221 waililia mahakama iwape hatimiliki ya shamba...

UKUMBI WA LUGHA NA FASIHI: Vikwazo vinavyokabili Kiswahili...

adminleo