• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Hii handisheki ni ndoto tu – Ruto

Hii handisheki ni ndoto tu – Ruto

Na SAMUEL BAYA

SIKU moja baada ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu Rais Uhuru Kenyatta na kinara wa ODM Raila Odinga kuungana, Naibu Rais William Ruto Jumamosi alisema muafaka huo utasalia ndoto na kumlaumu Bw Odinga, kwa kueneza siasa za utapeli na mgawanyiko.

Dkt Ruto alimtaja Bw Odinga kama kiongozi anayehubiri umoja huku akijihusisha na siasa za mgawanyiko kuanzia ndani ya chama chake cha ODM hadi katika chama tawala cha Jubilee.

“Ikiwa tunamaanisha kuunganisha Wakenya, basi matamshi yetu yanafaa kuwa sawa na vitendo vyetu. Hauwezi kudai kwamba unaunganisha Wakenya ilhali unachofanya ni kuwagawanya, kufukuza baadhi yao kutoka vyama vyao vya kisiasa na kuporomosha vyama vingine vya kisiasa,” Dkt Ruto alisema.

Akihutubia wakazi wa Ganze Kaunti ya Kilifi jana, Dkt Ruto alisema viongozi hawawezi kuunganisha Wakenya kupitia uongo, chuki na utapeli wa kisiasa.

Alilaumu chama cha ODM cha Bw Odinga kwa kumfukuza mbunge wa Malindi Aisha Jumwa akisema hatua hiyo haikuwa ya haki.

Bi Jumwa alifukuzwa na kutangaza kuwa atamuunga Dkt Ruto kugombea urais kwenye uchaguzi wa 2022.

Naibu Rais alisema hakuna mtu anayefaa kuomba ruhusa ya kushirikiana na serikali.

“Nilitazama kwa mshangao kiongozi wa chama akiitisha kongamano la chama kwa sababu anataka kumwadhibu mwanamke mmoja, kiongozi. Hawa watu wanafaa kuaibika,”

“ Ninataka kuwaambia kwamba chama chochote cha kisiasa au mwanasiasa yeyote anayepanga na kuanza kampeni dhidi ya viongozi wanawake hana nafasi Kenya katika karne ya ishirini na moja,” alisema Dkt Ruto.

Alisema kwamba iwapo viongozi wa chama cha ODM wanaamini wanaweza kuunganisha nchi kwa kugawanya chama cha Jubilee na kufukuza baadhi ya viongozi, wanajidanganya.

“Lazima tuseme ukweli. Kinachotendeka katika ODM ni siasa za utapeli na ukora na hadaa ya kisiasa ambazo hazina nafasi katika nchi hii,” alisema Dkt Ruto.

Aliongeza kuwa tatizo kubwa Kenya ni ukora wa kisiasa ambapo viongozi husema jambo moja na kutenda tofauti.

“Wanasema wanaunganisha Kenya ilhali wanachotenda ni kuwagawanya Wakenya,” alisema.

Matamshi yake yalijiri siku ambayo muafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na Bw Odinga ulitimiza mwaka mmoja.

“Wewe ni mwanamume sampuli gani unayeenda kupanga mkutano wa kumtimua mwanamke ilhali kuna viongozi wengi wanaume waliotoa matamshi sawa na ya mbunge huyo,” alisema akirejelea kutimuliwa kwa Bi Jumwa na chama cha ODM.

Alisema yeye na Rais Uhuru Kenyatta waliamua kuunganisha Wakenya kupitia Jubilee.

“Ninataka kusema nikiwa hapa Kilifi kwamba kama Wakenya na kama viongozi, tuliamua kuhamasisha Wakenya umuhimu wa kuishi pamoja kama taifa. Pia, tulizungumza na kukubaliana kumaliza ukabila na

Wakenya,” alisema.

Bi Jumwa alisema kuwa mwafaka kati ya Raila na Rais Uhuru Kenyatta hauna maana yoyote kwa sababu ulitumiwa kugandamiza wanasiasa wenye msimamo mkali kama yeye.

“Kile ambacho ninaweza kusema wazi kwamba Bw Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta waangalie upya hiyo handshake kwa sababu haijatusaidia popote, ” akasema Bi Jumwa.

You can share this post!

Kadhia ya moto mitaa ya mabanda Nairobi

Murkomen aitwa DCI kuhusu mabwawa

adminleo