• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 3:04 PM
Arsenal kupumzika Uarabuni wakati wa mechi za kimataifa

Arsenal kupumzika Uarabuni wakati wa mechi za kimataifa

NA CECIL ODONGO

KLABU ya Arsenal itakita kambi ya mazoezi na kucheza mechi ya kirafiki mjini Dubai wakati wa ziara ya siku tano nchini Saudi Arabia mwezi Machi.

Ziara hiyo itakuwa wakati wa kipindi cha mapumziko ya kimataifa kwa klabu za soka zinazoshiriki ligi mbalimbali duniani huku mechi hiyo ya kirafiki ikitarajiwa kuwakutanisha The Gunners na Al Nasr Dubai SC ya Uarabuni Jumanne Machi 26.

Mtanange huo utatumika kufungua uwanja mpya wa Al Maktoum uliojengwa kisasa  na utaanza saa 11 jioni, saa za Afrika Mashariki.

Wakati wa ziara hiyo ya haiba, kikosi cha kocha Unai Emery kitatembelea kituo cha kihistoria cha kimatibabu cha ugonjwa wa moyo wa Rashid na kasri la Naibu kiongozi wa mji wa Dubai ambaye pia ni Waziri wa Fedha wa Saudia,  Sheikh Hamdan bin Mohammed bin Rashid Sal Maktoum.

Mkufunzi wa Arsenal  Unai Emery anatarajiwa kutumia ziara hiyo kujifua kwa mechi za EPL zinazosalia haswa dhidi ya Newcastle April 1 itakayokuja tu baada ya mapumziko hayo.

“Itakuwa vizuri sana  kufanya mazoezi katika sehemu ambayo inaendelea kujivunia msimu wa majira ya joto nasi tukiwa na mazoea ya hali ya anga yenye ubaridi mwingi. Miundomsingi jijini Dubai ni mizuri sana na huwa ni ya kisasa, itakuwa hidaya kuwa katika ujumbe utakaoshiriki ufunguzi wa uwanja mpya wa kisasa wa soka mjini Dubai,” akasema Emery.

Mara ya mwisho Arsenali ilipopambana na Al Nasr ilikuwa Novemba 1976 ambako waliwapepeta mabao 3-1.

You can share this post!

Facebook kuzindua mbinu ya kusoma fikra za watu

Kagame na Museveni wazidi kupakana tope

adminleo