• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 2:07 PM
Afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza ukubwa wa uume

Afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza ukubwa wa uume

MASHIRIKA Na PETER MBURU

PARIS, UFARANSA

MWANAMUME bilionea aliaga dunia alipokuwa akifanyiwa upasuaji kwa ajili ya kuongeza ukubwa wa uume wake, alipovamiwa na mshtuko wa moyo katika hospitali moja Jijini Paris.

Bw Ehud Laniado, 65, alikuwa akifanyiwa upasuaji huo katika kliniki ya kibinafsi ambayo haikutajwa Jumamosi, wakati alizidiwa upasuaji ukiendelea na akakata roho.

Mfanyabiashara huyo wa Almasi alivamiwa na mshtuko wa moyo wakati kitu kilidungwa na kuwekwa katika uume wake, mashirika ya habari Ubelgiji yakaripoti.

Kampuni yake inayoitwa Omega Diamonds, iliyoko Jiji kuu la Ubelgiji, Antwerp lilithibitisha kuwa mfanyabiashara huyo amefariki.

Ujumbe kutoka kwa kampuni hiyo ulisema “Kiongozi mwenye maono, apumzike vyema. Kwa huzuni kuu tunathibitisha kuwa mwanzilishi wetu Ehud Arye Laniado amefariki.”

Lakini rafikiye mfanyabiashara huyo ambaye hakutaka kutajwa alisema kuwa Bw Laniado alikuwa mtu “aliyependa kuwa na mwonekano mzuri.”

Mfanyabiashara huyo anaripotiwa kuwa alimiliki baadhi ya biashara kubwa zaidi Monaco, pamoja na majumba ya kifahari.

Habari kwenye tovuti yake zilisema kuwa mwanamume huyo atasafirishwa hadi Israel kuzikwa huko.

Mnamo 2015, Bw Laniado aliuza almasi ghali zaidi duniani iliyoitwa Blue Moon kwa mfanyabiashara wa Hong Kong Joseph Lau Luen kwa Sh4.8 bilioni.

You can share this post!

Mwanamume aliyejifanya mwanamke abambwa

Lionesses kujaribu bahati tena ya kufuzu kushiriki Raga ya...

adminleo