• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 4:31 PM
Matiang’i aonya kuwaadhibu polisi wanaoua kiholela

Matiang’i aonya kuwaadhibu polisi wanaoua kiholela

NA MWANDISHI WETU

 WAZIRI wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i ameonya maafisa wa polisi watakaopatikana na hatia ya mauaji ya kiholela kuwa watawajibikia vitendo vyao kibinafsi.

Alisema wanaotenda uhalifu katika vikosi vya polisi hawatasazwa. Dkt Matiang’i alifichua kuwa, baadhi ya maafisa wakuu wa polisi katika eneo la Kisii tayari wanachunguzwa kwa kukiuka sheria zinazoongoza vikosi vya usalama nchini.

“Tunachunguza baadhi ya maafisa na hatua mwafaka itachukuliwa dhidi yao,” alisema.

Akiongea katika kipindi cha redio ya Egesa Jumatano asubuhi, Dkt Matiang’i alisema hakuna yeyote atayekiuka katiba atasazwa.

“Ninawahakikishia kuwa hatua itachukuliwa. Hatua hiyo yaweza kuwa kuachishwa kazi au kushtakiwa,” alisema waziri huyo huku akifafanua kuwa vitendo hivyo ni ukiukaji haki za kibinadamu.

Kumekuwa na malalamishi kuwa maafisa wa polisi wamekuwa wakishiriki mauaji ya kiholela huku wanaharakati na watetezi wa haki za kibinadamu wakitaka mauaji hayo kukomeshwa.

Na Ruth Mbula

Katika mkutano uliowahusisha wadau wakuu katika idara za haki na sheria jijini Nairobi, waziri Matiang’i alisema Kenya haina sera inayounga mauaji ya kiholela na madai kama hayo hayana msingi na ukweli wowote.

Alisema polisi hawajawahi kumwua yeyote kiholela kama mojawapo ya sera za humu nchini.

You can share this post!

Maboga yana manufaa mengi kiafya

Angaza FC yazidi kung’aa katika ulingo wa soka

adminleo