• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 11:05 AM
JAMVI: Huenda shinikizo za wandani wa Ruto kwa Uhuru zikamwondoa Raila kwa handisheki

JAMVI: Huenda shinikizo za wandani wa Ruto kwa Uhuru zikamwondoa Raila kwa handisheki

Na LEONARD ONYANGO

MATAMSHI ya wandani wa Naibu wa Rais William Ruto dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta yameibua maswali kuhusu ikiwa urafiki baina ya viongozi hao wawili wa Jubilee umeanza kupata nyufa.

Naibu wa Rais pamoja na wandani wake wamekuwa wakimshambulia kiongozi wa Upinzani Raila Odinga tangu alipotangaza kushirikiana na Rais Kenyatta mwaka mmoja uliopita.

Wanasiasa wa kambi ya Dkt Ruto wamekuwa wakikwepa kumshambulia Rais Kenyatta moja kwa moja.

Lakini katika siku za hivi karibuni wandani wa Dkt Ruto, wakiongozwa na Gavana wa Nandi Stephen Sang na wabunge Oscar Sudi (Kapseret) na Caleb Kositany (Soy), sasa wanaonekana kumvalia njuga Rais Kenyatta.

Viongozi hao wa Bonde la ufa wanadai kuwa vita dhidi ya ufisadi vinavyoendelea ni njama ya kutaka kusambaratisha azma ya Dkt Ruto kuwania urais 2022.

Naibu wa Rais naye amenukuliwa mara kadhaa akisema kuwa vita dhidi ya ufisadi vimegubikwa na siasa za 2022.

Kulingana na Dkt Ruto, urafiki baina ya Rais Kenyatta na Bw Odinga huenda ukasambaratisha chama tawala cha Jubilee.

Rais Kenyatta ameshikilia kuwa ataendelea kukabiliana na ufisadi na wahusika watachukuliwa hatua.

Bw Odinga, wiki iliyopita, alisema kuwa wanasiasa wandani wa Naibu wa Rais wanamshambulia bure.

“Rais Kenyatta bado amevalia sare ya Jubilee na mimi nimevalia sare ya ODM hivyo madai kwamba nitasambaratisha Jubilee hayana msingi,” akasema Bw Odinga alipokuwa akizungumza katika Soko la Toi mtaani Kibra, Nairobi alipoenda kuwaliwaza zaidi ya wafanyabiashara 1,900 ambao vibanda vyao viliteketea, Jumanne alfajiri.

Gavana Sang’ alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya mazishi katika eneo la Ziwa, eneobunge la Soy, Kaunti ya Uasin Gishu alimtaka Rais Kenyatta kusema kuelezea sababu zake za kutaka kumkwepa Dkt Ruto.

“Jamii ya Wakalenjin imekuunga mkono kwa muda mrefu. Mnamo 2002 ulipowania urais, jamii yako ilikukataa, Wakalenjin wakasimama na wewe. Katika uchaguzi wa 2013 na 2017 tumekuunga mkono na sasa unaonekana kutugeuka,” akasema Bw Sang’ huku akimrejelea Rais Kenyatta.

“Ikiwa unataka kutawala kwa muhula wa tatu tuketi chini tuongee na wala sio kutuhangaisha,” akaongezea.

Kulingana na mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha Nairobi Prof Edward Kisiang’ani, matamshi hayo ya wandani wa naibu wa rais ni ishara kwamba urafiki wa kisiasa baina ya Dkt Ruto na Rais Kenyatta umeanza kuyeyuka.

“Matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa na Ruto pamoja na wandani wake katika siku za hivi karibuni kuhusu vita dhidi ya ufisadi ni ishara tosha kwamba chama cha Jubilee kimeanza kupasuka.

“Matamshi hayo ni ithibati tosha kwamba uhusiano wa kisiasa baina ya Rais Kenyatta na Bw Ruto umefikia kiwango cha kushtua,” anasema Prof Kisiang’ani.

Mhadhiri huyo anasema itakuwa vigumu kwa chama cha Jubilee kusalia imara ikiwa viongozi wake watakuwa na misimamo tofauti kuhusiana na ufisadi.

“Huku Rais Kenyatta akiapa kukabiliana na ufisadi, kambi ya Naibu wa Rais imejitokeza na kupinga vikali. Nani ataachia atasalimu amri kwanza – Rais Kenyatta au Dkt Ruto?” anauliza Prof Kisiang’ani.

Kulingana na Prof Kisiang’ani matakwa ya Rais Kenyatta na yale ya naibu wake sasa hayapatani mithili ya mbingu na ardhi.

“Tatizo lililopo katika siasa ni kwamba huwa hakuna urafiki. Hakuna kulipa madeni wala kutimiza ahadi. Siasa ni ikiwa utapata matakwa yako ya kibinafsi,” anasema.

“Sasa wandani wa Ruto wameanza kumshambulia Rais Kenyatta moja kwa moja bila kujificha nyuma ya Bw Odinga,” anaongezea.

Matamshi ya wafuasi wa Naibu wa Rais William Ruto dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta yameibua maswali kuhusu ikiwa urafiki baina ya viongozi hao wawili wa Jubilee umeanza kupata nyufa.

Naibu wa Rais pamoja na wandani wake wamekuwa wakimshambulia kiongozi wa Upinzani Raila Odinga tangu alipotangaza kushirikiana na Rais Kenyatta mwaka mmoja uliopita.

Wanasiasa wa kambi ya Dkt Ruto wamekuwa wakikwepa kumshambulia Rais Kenyatta moja kwa moja. Lakini katika siku za hivi karibuni wandani wa Dkt Ruto, wakiongozwa na Gavana wa Nandi Stephen Sang na wabunge Oscar Sudi (Kapseret) na Caleb Kositany (Soy), sasa wanaonekana kumvalia njuga Rais Kenyatta.

Viongozi hao wa Bonde la ufa wanadai kuwa vita dhidi ya ufisadi vinavyoendelea ni njama ya kutaka kusambaratisha azma ya Dkt Ruto kuwania urais 2022. Naibu wa Rais naye amenukuliwa mara kadhaa akisema kuwa vita dhidi ya ufisadi vimegubikwa na siasa za 2022.

Kulingana na Dkt Ruto, urafiki baina ya Rais Kenyatta na Bw Odinga huenda ukasambaratisha chama tawala cha Jubilee. Rais Kenyatta ameshikilia kuwa ataendelea kukabiliana na ufisadi na wahusika watachukuliwa hatua. Bw Odinga, wiki iliyopita, alisema kuwa wanasiasa wandani wa Naibu wa Rais wanamshambulia bure.

“Rais Kenyatta bado amevalia sare ya Jubilee na mimi nimevalia sare ya ODM hivyo madai kwamba nitasambaratisha Jubilee hayana msingi,” akasema Bw Odinga alipokuwa akizungumza katika Soko la Toi mtaani Kibra, Nairobi alipoenda kuwaliwaza zaidi ya wafanyabiashara 1,900 wambao vibanda vyao viliteketea, Jumanne alfajiri.

Gavana Sang’ alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya mazishi katika eneo la Ziwa, eneobunge la Soy, Kaunti ya Uasin Gishu alimtaka Rais Kenyatta kusema kuelezea sababu zake za kutaka kumkwepa Dkt Ruto.

You can share this post!

JAMVI: Tuhuma za ufisadi huenda zikaathiri utendakazi wa...

JAMVI: Hofu ‘Tanga Tanga’ wanampumbaza Ruto...

adminleo