• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 8:27 PM
MAPISHI: Jinsi ambavyo unaweza kuoka keki ya karoti

MAPISHI: Jinsi ambavyo unaweza kuoka keki ya karoti

Na MARGARET MAINA

[email protected]

MUDA wa kuandaa: Dakika 20

Muda wa kuoka: Dakika 45

Walaji: 5

Vinavohitajika

  • Mayai 4
  • Butter kiasi cha kikombe kimoja na robo
  • Sukari nyeupe vikombe 2
  • Vanilla vijiko 2 vya chai
  • Unga vikombe 2
  • Baking powder vijiko 2 vya chai
  • Chumvi kiasi cha nusu kijiko cha chai
  • Cinnamon vijiko 2 vya chai
  • Karoti kiasi cha gramu 220
  • Baking soda kijiko 1
  • Nutmeg nusu kijiko cha chai
  • Buttermilk robotatu kikombe
  • Flaked coconut kikombe 1

Maelekezo

Washa ovena na dhibiti joto kwa nyuzijoto 350.

Kwenye bakuli weka unga, sukari, baking powder, baking soda, mdalasini, nutmeg, chumvi na kisha changanya vizuri sana. Weka pembeni.

Kwenye bakuli lingine weka mayai, siagi, vanilla na flaked coconut kisha koroga mpaka viwe laini kabisa.

Mchanganyiko wenye mayai mwagia kwenye unga kisha koroga mpaka vichanganyike vizuri.

Chukua karoti ulizoziandaa ukazikwangua. Ziweke kwenye mchanganyiko ule wa keki.

Koroga vizuri. Chukua chombo unachotumia kuokea keki yako kipake siagi.

Chukua mchanganyiko wa keki mwagia kwenye chombo hicho, weka kwenye ovena.

Baada ya dakika 45, funua uangalie kama keki imeiva.

Epuea. Ikishapoa, pakua kwa kuikata kwa mapande au vipande uvitakavyo na ufurahie na walaji wengine.

You can share this post!

AFYA: Umuhimu wa kunywa maji kila asubuhi

15 wasonga mbele Shield Cup, Ulinzi na Sofapaka zang’olewa

adminleo