• Nairobi
  • Last Updated March 28th, 2024 9:35 PM
Mswada kutua bungeni kutupa wafisadi ndani maisha

Mswada kutua bungeni kutupa wafisadi ndani maisha

Na CHARLES WASONGA

WATU ambao watapatikana na hatia ya makosa yanayohusiana na ufisadi huenda wakapewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani ikiwa bunge litapitisha mapendekezo ya mabadiliko kwenye sheria ya ufisadi.

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ameandaa mswada wa marekebisho ya Sheria kuhusu Mapambano dhidi ya Ufisadi unapendekeza kuwa watakaopatikana na hatia ya kushiriki uovu huo kufungwa jela kwa zaidi ya miaka 10.

Mbunge huyo wa Jubilee pia anapendekeza kuwa mali ya watu kama hao itwaliwe na watozwe kiwango cha juu cha faini, hatua ambayo anasema inalenga kupunguza vita dhidi ya ufisadi katika utumishi wa umma.

Bw Nyori anapendekeza kuwa faini iwe maradufu ya kiasi kilichoibiwa na gharama ya hasara inayosababishwa na ufisadi.

Kwa sasa, mtu ambaye hupatikana na hatia ya kushiriki ufisadi anaweza kutozwa faini ya kiwango kisichozidi Sh1 milioni au kifungo kisichazidi miaka 10 gerezani.

Mbunge huyo anapendekeza mabadiliko yafanyiwe sehemu ya 48 (1) ya Sheria kuhusu Ufisadi ili mtu atakayepatikana na hatua ya kushiriki uovu huo atozwe kiasi kisichopungua Sh1 milioni au kifungo cha muda usiozidi miaka 10 gerezani, au kifungo cha maisha.

Kulingana na mbunge huyo, hukumu ya sasa haiwezi kuzuia watu kushiriki ufisadi.

“Visa vya ufisadi vimeongezeka nchini na njia moja na kuzuia hali hiyo ni kuifanya adhabu ya uovu huo kuwa kali zaidi,” inasema mswada huo.

“Zimwi hili la ufisadi lisiposhughulikiwa, uovu huu utaendelea kuhujumu maendeleo kupitia wizi wa pesa za umma.”

Mswada huo wa marekebisho wa Sheria ya Ufisadi ya Uhalifu wa Kiuchumi unajri wakati ambapo serikali imeimarisha vita dhidi ya uovu huo katika sekta ya umma.

You can share this post!

Mvutano bungeni Keter akikataa kujibu maswali kuhusu mradi...

Mwanamke ampiga risasi mpenzi wake kwa kukoroma usingizini

adminleo