• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 6:55 AM
Maafisa wahamishwa kuzima unyakuzi wa ardhi

Maafisa wahamishwa kuzima unyakuzi wa ardhi

Na SAMMY KIMATU

BAADA ya agizo la Naibu Kamishena wa Kaunti Ndogo ya Starehe Kaunti ya Nairobi, Bw Kibet Boen walionyakua ardhi na kujenga nyumba juu ya kingo za mto Ngong kutoka Express Kenya hadi Mtaa wa mabanda wa Maasai na Kaiyaba wazibomoe, kufikia Jumapili hakuna aliyeonekana kubomoa jengo lake.

Fauka ya hayo, tingatinga lilianza kazi ya kufukua taka ndani ya mto huo karibu na kanisa la Liberty Pentecostal Church ndipo maji yateremke.

Bw Boen alikuwa amegadhabishwa na kile alichokiita ufisadi wa hali ya juu baada ya mabwenyenye kunyakua ardhi wakishirikiana na machifu kadhaa.

“Nimewahamisha maafisa waliokaa eneo hili kwa miaka kadhaa akiwemo Msaidizi wa Kamishena wa Kaunti South B, Bw Ahmed Barre aliyepelekwa Kangemi naye naibu wa chifu lokesheni ndongo ya Hazina, Bw Henry Emojong akahamishwa hadi Langata,” Bw Boen akasema.

Tingatinga lilianza kazi ya kufukua taka ndani ya mto huo karibu na kanisa la Liberty Pentecostal Church ndipo maji yateremke. Picha/ Sammy Kimatu

Baada ya maafisa hao kuhamishwa, wanaohudumu sasa ni Bw Philip Mbuvi anayechukua mahala pa Bw Barre huku naibu mpya wa chifu wa Hazina akiwa ni Bw Nelson Kambale.

Wakati wa kuzinduliwa kwa mpango wa kusafisha mto ili mafuriko yasiwe na makali kwa wazi, Bw Mbuvi alishikilia msimamo kwamba ni lazima watu wahame kutoka kingo za mto huo.

“Watu wameweka mchanga ndani ya magunia, wakazipanga kisha wakajenga nyumba juu yake na wanauliza serikali waytahamia wapi. Ni lazima watoke hapa la sivyo tinga tinga litabomoa lenyewe,” akasema Bw Mbuvi.

Alikuwa aeambatana na machifu Mabw Solomon Muranguri (Landmawe) na Charles Mwatha pamoja na wenyeviti wa mitaa ya mabanda katika eneo hilo.

You can share this post!

MALUMBANO: Wadigo mbona hatuwaelewi?

Burudani ya kipekee chuoni TUM Purity Nekesa akiibuka...

adminleo