• Nairobi
  • Last Updated March 29th, 2024 8:50 AM
KNH yasaka vipaji 15 kujisuka upya

KNH yasaka vipaji 15 kujisuka upya

Na JOIHN KIMWERE

TIMU ya Hospitali ya Kitaifa ya Kenyatta (KNH) imepania kutwaa huduma za wachezaji 15 wapya ili kujiweka pazuri kwenye mechi za Kundi A Ligi ya Taifa Daraja la Pili msimu huu.

”Nataka kupanga timu yangu vizuri maana kwenye kampeni za mkumbo wa pili tunatarajia mechi za mauano,” kocha wake, George Makambi alisema na kudai wachezaji wake waliokuwa tegemeo wamechotwa na klabu za Supa Ligi ya Taifa (NSL).

Aliambia Taifa Leo Dijitali kwamba kwenye mechi za msimu huu hakuna kulaza damu timu zote zinataka tiketi ya kusonga mbele. Alidokeza hayo muda mfupi baada ya timu yake kulimwa mabao 4-0 na Uweza FC Uwanjani KNH.

Mchezaji wa Kenafric FC (kulia) akishindana na mpinzani wa Uweza FC kwenye mechi ya Kundi A Ligi ya Taifa Daraja ya Pili. Mchezo huo ulitoka nguvu sawa mabao 2-2. Picha/ John Kimwere

Uweza FC ilivuna ufanisi huo kupitia Antony Munene, Austin Moya, Kofa Taplah na Kevin Njoroge. Nayo Balaji EPZ ilitoka sare tasa dhidi ya Mwiki United na kuendelea kuashiria zina kazi kubwa. Matokeo mengine, Kahawa United iliizaba Commercial mabao 2-0, Thunder Bird iliagana sare ya bao 1-1 na Magana Flowers. Kwenye jedwali, Balaji EPZ inaongoza kwa alama 22, moja mbele ya Mwiki United nayo KNH kwa kuzoa pointi 20 inafunga tatu bora.

Kocha wa Uweza FC, Charles ‘Stam’ Kaindi inayofunga tano bora kwa alama 17 hadi sasa siyo rahisi kubashiri ni timu gani itakayoibuka mabingwa wa msimu huu. ”Hakuna timu ya kupuuza zimejipanga vizuri kutifua vumbi la kufa mtu kung’ang’ania tiketi ya kupandishwa ngazi msimu ujao,” kocha huyo alisema.

You can share this post!

Thika Queens wajikuta njia panda KWPL

Makocha wa Zoo Youth na APs Bomet walenga makubwa

adminleo